HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 16 January 2019

RPC WANKYO AWAKOMALIA TRAFIK WAOMBA RUSHWA PWANI

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 
ASKARI wa usalama barabarani mkoa wa Pwani, wametakiwa kufanya kazi zao kwa weledi na kuacha kuomba na kupokea rushwa. Hayo yalisemwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Kamishina msaidizi Mwandamizi Wankyo Nyigesa ,wakati akizungumza na askari wa kikosi cha barabarani mkoa wa Pwani katika ukumbi wa Polisi Maisha plus Kibaha.

Alieleza yamekuwepo malalamiko kwa baadhi ya askari wa usalama barabarani kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa jambo ambalo limekuwa likichafua taswira ya Jeshi la Polisi.

"Katika kipindi cha uongozi wangu nitakuwa mkali na sitosita kuchukua hatua kwa askari yoyote atakayebainika kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa madereva"alisisitiza.


Aidha Wankyo,  aliwataka askari hao kuzingatia utoaji wa huduma bora kwa wateja wanaowahudumia kila siku na kuacha vitendo malumbano na majibu yasiyozingatia utu kwa wale wanaowahudumia katika barabara zetu.


Pia, aliwaasa ,madereva wanaoingia ndani ya mkoa wa Pwani kuzingatia sheria za usalama barabarani na wale watakaokaidi kutii sheria hizo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad