HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 30 January 2019

PRECISION AIR YAWA MSHIRIKA WA MASHINDANO YA KILIMANJARO MARATHONI


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Shirika la ndege linaloongoza Tanzanaia Precision Air limetangaza kuwa msafirishaji rasmi wa mashindano ya Kilimanjaro Marathon. Taarifa hiyo imetolewa na Meneja Masoko na Mahusiano wa shirika hilo Hillary Mremi kuwa wameamua kushiriki katika mashindano ya mwaka huu ili kuweza kuwezesha washiriki na watu wengine wanaoenda kufuatilia kupata fursa ya kwenda kwa bei rahisi.

Mashindano haya Kilimanjaro Marathon si tu kwamba yanasaidia kuinua vipaji vya wanariadha hapa nyumbani,lakini pia yanatangaza utalii kwa nchi yetu na Shirika la Precision Air kama wadau wakubwa wa utalii nchini wameamua kushiriki katika tukio hilo.

“Kilimanjaro Marathoni ni moja kati mbio za riadha zilizofanikiwa sana katika Ukanda wa Afrika Mashariki na ni furaha kubwa kwetu kua sehemu ya mashindano haya. Tukiwa kama shirika la Ndege linaloongoza Tanzania na tukiwa na safari zinazoiunganisha Kilimanjaro na Dar es Salaam, Zanzibar, Mwanza, Nairobi na Entebbe tumejizatiti kutoa usafiri wa anga wa haraka, uhakika na nafuu kwa wale wote wanaopanga kushiriki.” 

“ Tuna wasihii wale wanaopanga kuhudhuria Kilimanjaro Marathon mwaka huu, kuchangamkia fursa ya punguzo la nauli kwa safari zetu zote za ndani ya nchi, ambapo wanaweza kujipatia tiketi ya kwenda tu, kwa nauli ya kuanzia SH.90,000/-. Kupitia safari zetu 6 kati ya Dar es Salaam – Kilimanjaro, safari tatu kati ya Nairobi-Kilimanjaro, safari moja kati ya Mwanza – Kilimanjaro na safari moja kati ya Entebbe – Kilimanjaro abiria wetu watakua na uhuru mkubwa wakuchagua muda wa safari wakati wakipanga safari zao,"alisema Mremi

Mashindano ya Kilimanjaro Marathon ambayo yalianzishwa mwaka 2003 na kampuni ya Wild Frontiers yakiwa na lengo la kuutangaza utalii Tanzania yameendelea kukua na kuwa moja ya matukio makubwa ya kimichezo katika ukanda wa Africa Mashariki na Afrika nzima kwa ujumla. 

Akizungumzia udhamini wa Precision Air, Mkurugenzi wa Mbio hizo, John Addison amesema wanayofuraha kulikaribisha shirika hilo kama mshirika rasmi wa mashindano hayo. 

“Ushirikiano tunaopata kutoka kwa mashirika ya nyumbani kama Precision Air umesaidia kwa kiwango kikubwa kukuza hadhi ya mashindano haya na kuwezesha watu wengi zaidi kushiriki ikiwa ni pamoja na wanariadha na mashabiki watakao safari kuelekea Kilimanjaro kwa gharama nafuu kwa ajili ya kushiriki riadha pamoja na kusheherekea.” Alieleza Bw. Addison.

Meneja Masoko na Mahusiano wa Shirika la ndege linaloongoza Tanzanaia Precision Air Hillary Mremi akizungumza na waandishi wa habari kuelekea  mashindano Kilimanjato Marathoni na ushirika wao katika kusafirisha washiriki kwa bei nafuu.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad