Katibu
wa Makamu wa Rais Bw. Juma S. Mkomi akipokea Vifaa Tiba vya
kujifungulia wakina mama kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Meneja wa Benki
ya NMB Kanda ya Mashariki Bi. Aikansia Muro ikiwa sehemu ya Benki hiyo
kuunga mkono juhudi za Makamu wa Rais katika kuboresha huduma ya afya ya
Mama na Mtoto leo katika hospitali ya rufaa ya Morogoro ambapo Makamu
wa Rais alitoa zawadi kwa watoto 36 waliozaliwa tarehe 27, Januari kama
kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa.
Katibu wa Makamu wa Rais Bw. Juma S. Mkomi akimkabidhi Mwenyekiti wa
Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Morogoro Dkt. Lucy Nkya moja ya mabeseni
yenye mahitaji muhimu kwa watoto waliozaliwa leo ikiwa zawadi kutoka
kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan kwa watoto 36 waliozaliwa leo tarehe 27, Januari kama kumbukizi
ya siku yake ya kuzaliwa.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Morogoro Dkt. Lucy Nkya akionyesha juu
moja ya mabeseni yenye mahitaji muhimu kwa watoto waliozaliwa leo kama
ishara ya kumshukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka watoto 36 waliozaliwa leo
tarehe 27, Januari ikiwa ni kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo
Januari 27 kwa kushirikiana na Benki ya NMB, wametoa Vifaa Tiba vya
kujifungulia katika wodi ya Mama na Mtoto, pamoja na vifaa tiba hivyo
aliwazawadia watoto 36 waliozaliwa siku ya katika hospitali ya rufaa
ya mkoa wa Morogoro .
Makamu
wa Rais aliwakilishwa na Katibu wake Bw. Juma S. Mkomi ambaye amesema
kuwa Makamu wa Rais amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha huduma ya
afya ya mama na mtoto inaboreshwa.
“Suala
la kuboresha huduma ya mama na mtoto limeelezewa kwenye ilani ya
uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 lakini Makamu wa Rais kwa upekee
amelipa kipaumbele kwa sabau ni moja kati ya ahadi zake kuu wakati
kampeni” alisema Katibu huyo wa Makamu wa Rais.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Rita
Lyamuya amemshukuru Makamu wa Rais kwa kuwakumbuka watoto waliozaliwa
hospitalini hapo ambapo alisema kuwa watoto 36 wamezaliwa katika siku ya
leo na kwa kipindi cha robo mwaka watoto 1779 walizaliwa kati ya hao
waliozaliwa kwa upasuaji ni 586.
Aidha,
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Mashariki Aikansia Muro amesema Benki
ya NMB inaunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano katika
kuboresha huduma zote za kijamii hususani sula zima la afya na elimu na
wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha huduma za kijamii
ambapo leo wamemuunga mkono Mhe. Makamu wa Rais kwa kutoa Vitanda vinne
vya kujifungulia, Vifaa vya kumsaidia mama kujifungulia (delivery kit)
8, pamoja na vifaa vingine ambavyo kwa ujumla vinagharimu shilingi
milioni 5.
Kwa
Upande mwingine Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Bw. Clifford Tandari
ameishukuru Serikali kwa kutenga shilingi bilioni 8.5 kwa ajili ya
ujenzi wa hospitali 3 na vituo vya afya 11 katika mkoa wa Morogoro.
No comments:
Post a Comment