HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 9 January 2019

NAIBU WAZIRI AWATAKA BODI YA UTALII KUTUMIA WATU MAARUFU KUTANGAZA VIVUTIO

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
WIZARA ya Maliasili na Utalii imewaagiza bodi ya Utalii nchini (TTB) kutumia fursa ya watu maarufu na mashuhuri nchini ili kuweza kujitangaza zaidi. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu wakati alipokutana na menejimenti ya TTB jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa fursa kubwa ya kutangaza vivutio vya kitalii nchini ni kuwatumia watu maarufu kwakuwa wanakuwa na wigo mpana na ushawishi kwa jamii za watu mbalimbali wanaokuwa wanawafuatilia. Kanyasu ametolea mfano wa baadhi ya wachezaji wa mpira wa miguu wanaocheza soka la kulipwa nje ya ukanda wa Afrika na hata wale waliokuwa ndani ya ukanda kuwatumia ili kufanikisha adhma ya kufikia watalii milioni 2 ifikapo 2020.

Ameeleza kuwa mbinu nyingine ya kuweza kujitangaza zaidi ni kuwapa mialiko watu mashuhuri hususani wakimbiaji wa riadha wa kimataifa ili kuja kushiriki katika mbio mbalimbali zinazokuwa zinafanyika Mkoani Arusha. “Kuutangaza utalii ni gharama kubwa sana ila lazima utumie fedha nyingi ili uweze kuingiza fedha zaidi, tunafahamu ufinyu wa bajeti kwa upande wenu ila tutajitahidi na kushirikiana nanyi katika kuhakikisha utalii unakuwa siku hadi siku,” amesema Kanyasu.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa TTB Devotha Mdachi amesema kuwa wameshafanya mazungumzo na baadhi ya watu mashuhuri akiwamo Mbwana Samatta na Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ ili kuwa mabalozi wa hiari kwa kututangazia vivutio vya nchini. Amesema mbali na hilo pia wana watu wengine tayari wameshakuwa mabalozi wa hiari akiwamo Yusuph Poulsen ambaye ni kijana mwenye asili ya kitanzania na wengine kutoka China na maeneo mengine.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu akizunguma na wanahabari sambamba na kutoa maagizo kwa bodi ya utalii nchini TTB wakati alipotembelea ofisi zao

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad