HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 14 January 2019

MWANACHUO NCHINI MISRI AFUKUZWA CHUO KWA KUMKUMBATIA MWANAUME HADHARANI

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MWANAMKE mmoja nchini Misri amefukuzwa chuo baada ya kuonekana akimkumbatia mwanaume katika moja ya video iloyosambaa katika mitandao.

Binti huyo amefukuzwa katika chuo cha Al -Azhar akishutumiwa kujidharilisha yeye na chuo baada ya kuonekana akimkumbatia mwanaume huyo katika video ambayo ilichukuliwa katika chuo cha Mansoura nchini humo.

Baraza la nidhamu la chuo cha Al- Azhar lililokaa siku ya jumamosi liliamua kumfukuza Chuo binti huyo, Msemaji wa baraza hilo Ahmed Zarie alieleza vyombo vya habari.

Imeelezwa kuwa video hiyo imeleta picha mbaya kwa chuo hicho kitu ambacho hakiruhusiwi aidha imefahamishwa kuwa kukumbatiana baina ya mwanamke na mwanaume ambao hawajaolewa sio maadili wala taratibu za jamii ya taifa hilo.

Kwa upande wa kijana aliyeonekana kwenye video, msemaji wa baraza hilo amesema kuwa watakaa leo jumatatu na kufanya maamuzi dhidi yake. 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad