HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 24 January 2019

MIRADI YA TEDAP YAIMARISHA UPATIKANAJI,USAMBAZAJI UMEME KWA WATEJA ARUSHA

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
SHIRIKA la Umeme Tanzania(TANESCO)limesema kwamba kutekelezwa kwa mradi wa Kukarabati na Kuimarisha Mifumo ya Umeme Tanzania(TEDAP) umesaidia kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika hasa katika mikoa mbalimbali ambayo TEDAP inatekelezwa.

Kwa Mkoa wa Arusha TEDAP imesaidia kuufanya mkoa huo kuwepo kwa umeme wa uhakika na kwamba kutokana na ukarabati na uimarishwaji wa mifumo ikiwemo ya usambazaji umeme imeifanya TANEACO Mko wa Arusha kuwa na umeme wa unaotesheleza wateja na kuwepo na akiba ambayo haitumiki.

Akizungumzia utekelezaji wa TEDAP Mkoa wa Arusha,  Menaja Mwandamizi wa Miradi kutoka Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) Mhandisi Emmanuel Manirabona amesema katika mkoa huo kuna mafanikio makubwa na kwamba ndio maana wanahamasisha watu wawekeze kwani kuna umeme wa uhakika.

Amefafanua kupitia TEDAP wamerabati kituo cha umeme cha Mt.Meru, kituo cha Njiro B, kituo cha Sakina, kituo cha Themi, kituo cha Unga Ltd, kituo cha T/School na Kituo cha Kiltx.na kwamba uwepo wa vituo hivyo na uboreshwaji wake umeongeza ufanisi  wa utoaji huduma ya nishati ya umeme kwa wateja wao.

"Kutekelezwa kwa TEDAP ndani ya Mkoa wa Arusha umepiga hatua kubwa ya upatikanaji wa umeme wa uhakika,leo hii Arusha hata malalamiko ya wateja yamepungua kwani hata tatizo la kukatika kwa umeme halipo kama ilivyokuwa huko nyuma," amefafanua.

Mhandisi Manirabona amesema kupitia miradi ya  TADEP imesaidia kuifanya TANESCO kufanya kazi zake kwa uharaka zaidi hata pale linapotokea tatizo la umeme kupitia mitambo iliyopo inasaidia kupata taarifa ya tatizo la umeme kabla ya mteja kufika ofisi za shirika hilo kutoa taarifa.

"Kuna mitambo ya kisasa ambayo yamerahisisha hata upatikanaji wa taarifa.Chochote ambacho kinafanyika katika mfumo wa umeme tunapata taarifa kwa haraka sana," amefafanua Mhandisi Manirabora huku akisisitiza watu kujenga viwabda Arusha kwani umeme wa uhakika.

Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa Modumo ya Usambazaji Umeme kituo cha usambazaji umemenNjiro Rembrice Mollel ameto ufafanuzi kuhusu namna mifumo ilivyo kwenye kituo hicho namna ambavyo imeboreshwa na hatimaye kirahisisha utoaji huduma ya nishati ya umeme.

Pia amesema kwamba katika kituo hicho wanazo njia tatu za kusambaza uneme ambapo njia moja ni ya 220 kilovolti na njia nyingine mbili za kusambaza umeme zina uwezo wa 132 kilovolti kwa  kila mmoja.

",Katika kituo hiki cha Njiro hatuna tatizo kabisa la umeme,wateja wetu wanapata umeme wa uhakika na usiokatika.Kupitia," amesisitiza huku akifafanua kwa mifumo ya usambazaji umeme waliyonayo ni ya kisasa na hivyo inawarahisiahia katika kutoa huduma kwa wateja.
 Meneja wa Mradi wa Shirika La Umeme TANESCO, Mhandisi Emmanuel Marinabona akielezea jambo wahariri na waandishi waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini kuhusu hatua mbalimbali ambazo mradi wa TEDAP ulipitia kukamilisha upanuzi wa miundo mbinu ya kusambaza umeme na kupunguza changamoto mbalimbali za umeme katika Mkoa wa Arusha leo. Mradi huo unahusisha vituo sita vya umeme pamoja na kituo kikuu cha kusambaza umeme cha Njiro. 
 Kaimu Meneja wa Uhusiano wa shirika la umeme TANESCO, Leilah Muhaji akijibu maswali aliyoulizwa na waandishi wa habari kuhusu hatua mbalimbali ambazo mradi wa TEDAP ulipitia kukamilisha upanuzi wa miundo mbinu ya kusambaza umeme na kupunguza changamoto mbalimbali za umeme katika Mkoa wa Arusha leo. Mradi huo unahusisha vituo 6 vya umeme pamoja na kituo kikuu cha kusambaza umeme cha Njiro. 
Mkuu wa Usambazaji Umeme Mkoa wa Arusha, Mhandisi Donasiano Shamba akielezea jambo wahariri na waandishi waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini kuhusu hatua mbalimbali ambazo mradi wa TEDAP ulipitia kukamilisha upanuzi wa miundo mbinu ya kusambaza umeme na kupunguza changamoto mbalimbali za umeme katika Mkoa wa Arusha leo. Mradi huo unahusisha vituo 6 vya umeme pamoja na kituo kikuu cha kusambaza umeme cha Njiro. 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad