HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 29, 2019

KUENDELEA KUTUMIA SHERIA KANDAMIZI KWA BAADHI YA NCHI ZA AFRIKA NI VYANZO VYA KUMDIDIMIZA MWANAWAKE

NA, VERO IGNATUS -ARUSHA.
Kundelea kutumika kwa sheria kandamizi kwa wanawake na watoto katika baadhi ya nchi barani afrika kumetajwa kuwa miongoni mwa vyanzo vinavyo mdidimiza mwanamke kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kumnyima haki mbalimbali ndani ya jamii.

Hayo yamesemwa na mtaalamu wa masuala ya sheria zinazo husu haki za wanawake na watoto kutoka umoja wa mataifa wanawake (UN-WOMEN) Bi Rachel Boma jijini Arusha ambapo amesema matumizi ya sheria kandamizi yamekuwa yakimdhofisha mwanamke katika kuleta mabadiliko kuanzia ngazi ya familia.

Hali hiyo inawakutanisha shirika la umoja wa mataifa wanawake (UN-WOMEN) kwa kushirkiana  na chama cha majaji na mahakimu wanawake Tanzania (TAWJA) kwa lengo la kubadilishana uzoefu ikiwa ni pamoja na kuona namna ya kumuwezesha na kupaza sauti mwanamke katika msaada wa kisheria na haki kwa wanawake barani afrika.

Na hapa bi Joaquine De Mello ambae ni Jaji Mahakama Kuu nchini Tanzania amesema changamoto zinazo mkabili mwanamke katika muktadha wa kisheria ambapo changamoto za mila na desturi zimekuwa kikwazo katika kutetea haki za wanawake jambo ambalo linahitaji ushiriki mpana.

Jaji Mello amesema kuwa sheria za ndoa, sheria ya miradhi inapaswa kuangaliwa upya kwani vipo baadhi ya vipengele vinavyomkandamiza mwanamke na zinamnyima haki zakeza msingi.

Dkt Gerald Ndika ni jaji wa mahakama ya rufani amesema kwa sasa wataalamu wa sheria wamekuwa wakiendelea kutoa elimu kuhusu msaada wa kisheria kwa ajili ya kusisitiza haki kwa mtoto na mwanamke bila kujali uwezo wa kifedha.

Aidha Dkt  Gerald amesema kuwa juhudi endelevu zinahitajika kupiga vita vitendo vyq unyanyasaji wawanawake pamoja na kutathmini utekelezaji wa mikataba hiyo ili iweze kuzaa matunda.

Kwa mujibu wa wataalamu hao wa masuala ya kisheria imeelezwa kuna haja ya kufanya marekebisho katika baadhi ya vipengele vya sheria ya ndoa na mirathi kwa maslahi ya kuthamini nafasi ya mwanamke katika kuchochea maendeleo katika jamii.

Picha :Mtaalamu wa Masuala ya Sheria zinazo husu haki za wanawake na watoto kutoka umoja wa Mataifa Wanawake (UN-WOMEN) Bi Rachel Boma

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad