HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 3, 2019

KESI YA MBOWE NA WENZAKE YAPIGWA KALENDA TENA

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii.
Wakili wa upande wa mashtaka Katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe  na viongozi wenzake nane,  Process Abdallah Safari ameuhoji upande wa mashtaka iwapo rufaa waliyokata Mahakama ya rufaa ilikuwa chini ya hati ya dharura na kama Hawakufanya  hivyo ni kwa nini.

Hatua hiyo imekuja baada ya wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi kuieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kesi  hiyo leo January 3.2019 imekuwa kwa ajili ya kutajwa. Akijibu Awali hilo, wakili Kadushi amedai, hakuna uhalali wa kisheria kuhusu swali hilo mahakamani hapo, labda lingeulizwa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufaa

Katika kesi hiyo  inayounguruma mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,  Wilbard Mashauri,  Mbowe, na Mbunge wa Tarime mjini, wanasota eyande baada ya kukiuka masharti ya dhamana na kufutiwa dhamana yao hiyo.

Mbowe na Matiko watandelea kusota rumande hadi tarehe tajwa kufuatia Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam kusimamisha usikilizwaji wa rufaa iliyokatwa na upande wa mashtaka wakipinga maamuzi ya Mahakama ya Mahakama Kuu ya kusikiliza rufaa iliyowasilishwa ya na washtakiwa kudinga kufutiwa kwao dhamana.

 Novemba 26, 2018 Washtakiwa hao walifutiwa dhamana zao baada ya kukiuka masharti ya dhamana. Baada ya mabishano kidogo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi January 17,2019 huku akisema swali hilo la rufaa wakalihoji Mahakama Kuu.
 
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya  na Katibu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu 

Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya February Mosi na 16,  mwaka huu maeneo ya  Dar es Salaam.



Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe akitoka mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kurejea rumande mara baada ya kesi yake kuahirishwa na kutajwa tena january 17 /2019.
Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe akiwa na washtakiwa wenzie akizungumza na Wakili wake Prof Award Safari.
Mbunge wa Kibamba kupitia Chadema, John Mnyika, akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Vicent Mashinji mara baada ya kutoka katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akitoka nje ya jengo la Mhakama mara baada ya kuahirishwa kwa kesi inayowakabili katika mahakama hiyo.
Baadhi ya Viongozi Waandamizi wa Chadema wakitoka katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi ya Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad