HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 8, 2019

BENKI YA MAENDELEO (TIB) YATEULIWA KUWA MWENYEKITI KAMATI NDOGO YA TAASISI ZA FEDHA SADC, YAORODHESHWA KAMA TAASISI BORA ZA MAENDELEO BARANI AFRIKA

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
BENKI ya maendeleo ya TIB imechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ndogo ya taasisi za fedha za maendeleo ya jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa muda wa miaka miwili na kuhaidi ushirikiano pia amewataka watanzania kutumia fursa hiyo katika biashara na ushirikiano.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya taasisi ya fedha za maendeleo za ukanda wa SADC Charles Singili amesema kuwa aliteuliwa nafasi hiyo mwezi Disemba mwaka jana na atahudumu nafasi hiyo kwa miaka miwili, kuanzia Disemba 2018 hadi Disemba 2020.

Singili amesema kuwa uteuzi huo ni muhimu kwa taifa na kwa benki ya maendeleo TIB pamoja na Serikali kwa ujumla na amewahimiza  wananchi kutumia fursa hiyo kwa kuwa kuna viongozi wanaoshikilia nafasi muhimu katika jumuiya ya SADC akiwemo Rais Dkt.John Magufuli ambaye ni Makamu Mwenyekiti  wa marais wa jumuiya hiyo na Agosti 2019 Rais Magufuli atashika usukani kama Mwenyekiti wa SADC pia Katibu mkuu wa sasa wa jumuiya hiyo Dkt. Stergomena Tax ambaye  ni mtanzania pia.

Aidha Singili amesema kuwa hiyo ni nafasi pekee kwa Tanzania hivyo lazima majukumu yapokelewe na kuchapa kazi ili kuwa chachu ya maendeleo katika ukanda wa maendeleo kusini mwa Afrika. Aidha amesema kuwa Benki ya maendeleo TIB itatumia fursa hiyo kuhamasisha taasisi za fedha nchini na zile za nchi wanachama wa SADC katika kuhakikisha miradi ya maendeleo yenye maslahi ya kikanda inatekelezwa na hiyo ni pamoja na usafiri, nishati, maji na kuhakikisha fedha za kutosha zinapatikana.

Kuhusiana  fursa watakazozipa kipaumbele  Singili amesema kuwa watashirikiana na taasisi nyingine kwenye mtandao ili kuwezesha maandalizi ya miradi inayokopesheka kwa kutumia mfuko wa SADC wa kuandaa miradi mbalimbali.

Pia Benki ya TIB itashirikiana na serikali na taasisi binafsi katika kujenga mazingira wezeshi kwa Tanzania hasa kwa kusaidia nchi kupata rasilimali fedha na kuwezesha utekelezaji wa miradi na kubwa zaidi ni kuendana na idhini ya serikali kwa kuwezesha miradi yenye manufaa kwa ukanda wa SADC pamoja na kupata wadhamini kutoka taasisi za fedha za SADC.

Vilevile Singili Singili ametoa taarifa ya mwenendo wa benki hiyo ambapo amesema kuwa taasisi za fedha za maendeleo ya Afrika (AADFI) iliitangaza benki ya TIB kwa kupata asilimia 80 (daraja A) na kupata heshima ya kuorodheshwa katika jedwali la heshima la Afrika.

Singili amesema kuwa benki ya TIB imekuwa ikifanya vizuri katika utawala bora na makundi ya uendeshaji na hiyo ni kutokana na usimamizi wa benki, bodi na timu ya wafanyakazi. Amehaidi kufanya kazi na serikali ili kuendelea kuongeza rasilimali zaidi kwa kufadhili miradi ya maendeleo katika kujenga uchumi wa viwanda nchini.
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Fedha za maendeleo za ukanda wa SADC Charles Singili akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uteuzi wa benki hiyo uliofanya Disemba mwaka jana pamoja na heshima iliyopata Benki hiyo kwa kuwekwa kwenye jedwali la heshima baada ya kupata daraja A katika masuala ya utawala bora na makundi ya uendeshaji tuzo iliyotolewa na taasisi ha AADFI, leo jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad