HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 30, 2019

AIRTEL KUENDELEA KUSHIKIANA NA JESHI LA POLISI

Na Jeshi la Polisi.
Kampuni  ya  simu za mkononi ya Airtel imelipongeza  Jeshi la Polisi  kwa ushirikiano mkubwa wanaoipatia  katika suala zima la ulinzi wa  raia na mali zao jambo ambalo linawezesha kampuni  ya Airtel kuendelea kutoa huduma kwa watanzania.
 Mkurugenzi  Mtendaji  wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Sunil Colaso  alitoa shukrani kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro  na Mkoa wa kipolisi Kinondoni kwa kusaidia kuwakamata na kuwafikisha mahakamani  wahalifu  waliotaka kuiba fedha  zaidi ya shilingi  bilioni moja  kutoka kampuni simu ya Airtel.
Aliongeza kuwa Kampuni yake itaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika mawasiliano ili wananchi waendelee kupata huduma ya ulinzi na  usalama.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro alimpongeza Mkurugenzi  Mtendaji  wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Sunil Colaso  kwa kuleta mrejesho wa kazi nzuri inayofanywa  na Jeshi la Polisi na kuongeza kuwa ni watu wachache wanaokuwa tayari kuleta mrejesho wa kazi nzuri inayofanywa na  Jeshi la Polisi.
Vilevile,   IGP Sirro aliwataka maofisa wote wa Polisi kuiga mfano wa Kamanda wa mkoa wa Kipolisi Kindondoni ili kujenga na kulinda taswira nzuri ya Jeshi la Polisi kwa kuwa kazi yao ni kuhakikisha wahalifu wote wanashughulikiwa  kwa mujibu wa sheria.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akizungumza na Mkurugenzi  Mtendaji wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Sunil Colaso pamoja na maofisa wa kampuni hiyo walipofika ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwa lengo la kutoa shukrani na pongezi kwa Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni kwa kufanikisha kuwakamata wahalifu waliotaka kuiba zaidi ya shilingi bilioni moja kutoka Airtel.      
( Picha na Jeshi la Polisi.)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad