HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 29 December 2018

YANGA YAENDELEZA UBABE TPL, YAIFUNGA MBEYA CITY 2-1 SOKONE MBEYA

Na Ripota Wetu, Mbeya
Timu ya Yanga imeendelea kushikilia usukani wa ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Mbeya City mechi iliyochezwa kwenye dimba la Sokoine Jijini Mbeya.
Yanga wamefanikiwa kuibuka ushindi huo na kufikisha alama 50 akiwa amecheza michezo 18 akishinda 16 na kutoa sare michezo miwili.

Katika dakika ya 16 Mshambuliaji wa Kimataifa Heritier Makambo anaiandikia Yanga goli la kwanza akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Ajib baada ya madhambi kutokea nje ya 18.

Dakika ya 24, Mbeya City wanasawazisha goli kupitia kaa Msambuliaji wake Iddy Seleman 'Nado' na kuanza kulisakama lango la wapinzani wao ili wapate goli la kuongoza.

Makambo akiwa ndani ya eneo la hatari aliweza kuwainua mashabiki wa Yanga katika dakika ya 41 akiwapeleka wana jangwani hao mapumziko wakiwa wanaongoza kwa goli 2-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Mbeya City wakisaka goli la kusawazisha lakini umakini wao ukiwa mdogo na kushindwa kutumia nafasi walizozipata.


Mpaka filimbi ya mwisho ya mwamuzi Martin Sanya inapigwa Yanga anatoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 2-1 akiendelea kushikilia rekodi ya kutokufungwa.
Kiungo wa Yanga Feisal Salum 'Fei Toto'  na Haruna Moshi 'Boban' wakiwania mpira na mchezaji wa Mbeya City  Mpoki Mwakinyuke wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Kiungo wa Yanga Feisal Salum 'Fei Toto'  na Haruna Moshi 'Boban' wakiwania mpira na mchezaji wa Mbeya City  Mpoki Mwakinyuke wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Mchezaji wa Mbeya City Medson Mwakatundu akiwa anaoambana kuchukua mpira kutoka kwa Heritier Makambo wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Kazi kaziniiiiii............................Heritier Makambo na Medson Mwakatundu
Mchezaji wa Mbeya City Mpoki Mwakinyuke akiondosha mpira mbele ya Mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngasa wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Picha zote na Fadhil Attik Teammapicha Mbeya


No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad