HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 18 December 2018

WIMBO WA MWANZA WAWAPONZA DIAMOND NA RAYVAN WAFUNGIWA KWA MUDA USIOJULIKANA

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limetangaza kumfungia mwanamuziki Nasibu Abdul (Diamond Platnumz) na Raymond Mwakyusa (Rayvan) kutokana na kitendo chake cha kupuuzia.

Basata imesema Diamond na Rayvan wamepuuzia na kuendelea kuutumia wimbo wa “Mwanza” maarufu kama Nyegezi katika shoo zake za Wasafi Festival na kuonesha dharau na  utovu wa nidhamu kwa mamlaka zinazosimamia masuala ya sanaa nchini na uvunjifu wa maadili uliokithiri.

Katika barua iliyotolewa leo mapema, Basata wameeleza pia kuwa wamewafungia wasanii hao kutokufanya shoo ndani na nje ya nchi kwa kipindi kisichojulikana kuanzia Desemba 18 2018.

Pamoja na hayo Basata wamefuta kibali cha Tamasha la Wasafi Festival kutokana na ukiukwaji wa Sheria, Kanuni na Utaratibu katika uendeshaji wa tamasha hilo hapa nchini.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad