HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 7, 2018

WAZIRI LUGOLA AMBANA AFISA ELIMU KWA KUKATAA KUANDIKISHA WANAFUNZI DARASA LA KWANZA

 Mwandishi Wetu, MARA.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza kutokuandikishwa mpaka wazazi wao walipe michango wanaodaiwa katika shule mbalimbali jimboni kwake Mwibara, Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara.  Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, amemtaka Afisa Elimu wa Kata ya Chitengule, Jimboni humo, Thadeo Lukinisha kuruhusu shule za msingi zilizopo katika Kata yake kuandikisha wanafunzi hao bila kikwazo chochote kwakuwa elimu ya shule ya msingi ni bure nchi nzima.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Nakatuba katika Kata hiyo, Lugola alipiga marufuku utaratibu huo ambao amesema hauna msingi wowote kwasababu unawaonea watoto ambao hawana kosa lolote hata kama kuna madeni ambayo wazazi wa wanafunzi hao wanadaiwa kutokana na watoto wao wanaoendelea na masomo katika shule zilizopo jimboni humo.  “Huu utaratibu sio sawa, haukubaliki, kipindi hiki wanafunzi wanaandikishwa kuanza darasa la kwanza waandikishwe bila kikwazo chochote ili waweze kupata elimu yao kama inavyostahili, michango yenu haihusiani na wanafunzi kuanza shule,” alisema Lugola. 

Hata hivyo, Afisa Elimu huyo tukio hilo lipo lakini walifanya hivyo kutokana na baadhi ya wazazi kutolipa kiasi cha shilingi mia nne ambayo inachangwa kwa ajili ya kila mwanafunzi anachangia kwa ajili ya kumlipa mpishi pamoja na mafuta ambayo fedha hiyo inalipwa kwa mwaka. Lugola alipata taarifa hiyo ya wazazi kukataliwa kuandikishwa watoto wao kuanza darasa la kwanza, baada ya mzazi mmoja kuulalamikia utaratibu huo na kuwafanya wazazi kutokuanidisha watoto hao kutokana na kudaiwa michango hiyo.

“Sitaki kusikia hili, Afisa Elimu huu sio utaratibu sahihi, lazima watoto waandikishwe kuanza masomo, na niwataka wazazi wote wahakikishe watoto wao wanaandikishwa haraka iwezekanavyo,” alisema Lugola huku akishangiliwa na wananchi waliohudhuria mkutano huo. Kwa upande wake Afisa Elimu huyo baada ya kauli ya Waziri Lugola aliwaelekeza walimu wa shule zilizopo katika Kata hiyo waweze kaundikisha watoto wao bila kikwazo chochote. 

“Napenda kutangaza kuwa, kuanza sasa wanafunzi waandikishwe bila kikwazo chochote katika shule ya Nakatuba na zinginezo ndani ya Kata hii ya Chitengule,” alisema Lukinisha.  Shule zilizopo katika Kata hiyo wanapewa chakula cha msaada na Shirika lisilokua la Serikali la PCI ambapo wazazi uchangia fedha kidogo ya mafuta na ya mlinzi hivyo uliwekwa utaratibu wa kila mwanfunzi katika shule hizo wachange shilingi 400 ili ziweze kuchangia huduma hizo.

Lugola anaendelea na ziara yake kwa kutembelea vijiji vyote jimboni kwake Mwibara akisikiliza kero za wananchi pamoja na kuhamasisha kilimo cha mazao ya pamba, mahindi, mpunga, viazi na mengineyo ambayo wakazi wa jimbo lake wanalima mazao hayo kwa wingi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimsalimia Mkazi wa Kijiji cha Namalebe, Kata ya Chitengule, Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda, Kaswanila Molore kabla ya kuanza mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kijiji hicho. Akizingumza na wananchi wa Kata hiyo, Lugola amepiga marufuku wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza kutokuandikishwa mpaka wazazi wao walipe michango wanaodaiwa katika shule mbalimbali jimboni humo. Na Mpiga Picha Wetu
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad