HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 19 December 2018

Watanzania waaswa kuwa wamoja

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akionyesha Tuzo ya Heshima aliyopewa Rais Dkt. John Magufuli na Jumuiya ya Maridhiano wakati wa Dua Maalumu ya Kumuombea Rais kwa kutimiza Miaka mitatu madarakani na Kuombea Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiyahiyo, Asha Kassim. Maombi hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa Dua Maalumu ya Kumuombea Rais kwa kutimiza Miaka mitatu madarakani na Kuombea Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa.Kulia ni Askofu Silvestre Gamanywa na Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania iliyoandaa maombi hayo, Asha Kassim.Maombi hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Sabasaba, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Sheikh Nurdin Mangochi akizungumza wakati wa Dua Maalumu ya Kumuombea Rais kwa kutimiza Miaka mitatu madarakani na Kuombea Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa..Maombi hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
 Askofu Silvestre Gamanywa akizungumza wakati wa Dua Maalumu ya Kumuombea Rais kwa kutimiza Miaka mitatu madarakani na Kuombea Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa.Maombi hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa dini wakiwa katika Dua Maalumu ya Kumuombea Rais kwa kutimiza Miaka mitatu madarakani na Kuombea Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa. Maombi hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Sabasaba, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Na Mwandishi Wetu
Watanzania wametakiwa kuwa wamoja na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kwa kumuombea  dua  katika kipindi hiki ambacho nchi inapitia kipindi cha mabadiliko makubwa ya kiuchumi huku Serikali ikikataa kupokea misaada yenye masharti ya kudhalilisha mila na desturi za Watanzania.

Hayo  yamesemwa  na  Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad  Masauni,  wakati akimuwakilisha Rais  Dkt. John  Magufuli katika  Dua  Maalumu ya Kumuombea  Rais Magufuli na Kuombea Amani Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa, iliyoandaliwa  na  Taasisi  ya Kidini ya Maridhiano  Tanzania, katika Ukumbi wa Mikutano wa Sabasaba,jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa maombi hayo Naibu Waziri Masauni alisema nchi sasa inapitia kipindi cha mabadiliko makubwa ya kiuchumi yanayosimamiwa na Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli lengo ikiwa ni kuifanya Tanzania isiwe tegemezi na kupewa masharti yanayodhalilisha mila, tamaduni na dini zetu.

“Watanzania tumuunge mkono Rais Magufuli, anayoyafanya ni kwa faida ya Watanzania wote bila kujali dini, rangi, kabila au itikadi na hatutakuwa tayari kupangiwa na wageni ambao wanatuletea mambo ya hovyo,demokrasia ya nchi yetu tunaijua wenyewe Watanzania na sio aje mtu kutoka nje atuambie demokrasia ya kufuata, hawezi kuja mtu atupangie tufuate mambo ya ushoga,” alisema Masauni

Akizungumza katika dua hiyo, Sheikh Nurdin Mangochi aliwataka Watanzania waitunze amani iliyopo na wala wasikubali kushawishiwa na mtu yoyote kuvuruga amani iliyopo.

“Kuna nchi jirani amani imetoweka na tunaona madhara yake, muhimu hii amani tuliyonayo tuitunze na kuilinda kwani nchi yetu Tanzania imekua darasa la amani kwa nchi jirani wanaokuja kujifunza jinsi Watanzania tunavyoishi bila kuwepo machafuko,” alisema Sheikh Mangochi

Naye Askofu Silvestre Gamanywa aliwataka Watanzania kuwa na Uzalendo na nchi yao kwa kuiongelea mema nchi katika maisha yao yote hali itakayopelekea kuwapo na mapenzi ya nchi kwa kila mtanzania.

“Uzalendo sio lazima kufia nchi yako,uzalendo ni kuwa na mtazamo chanya wa kuisemea na kuitetea nchi yako pamoja na kuitalia mema  na sio kuiongelea vibaya,” alisema Askofu Gamanywa.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad