HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 18, 2018

Wananchi waaswa kuwafichua Wahamiaji Haramu

Serikali imewaasa wananchi kutoa taarifa za kuwepo wahamiaji wanaoishi maeneo mbalimbali  nchini kinyume na sheria  za nchi ili raia wema waweze kufanya shughuli za maendeleo kwa amani na salama huku ikiwaasa watumishi wa Idara ya Uhamiaji kuwa waadilifu katika maeneo yao ya kazi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja yenye kauli mbiu ya Uhamiaji Unaozingatia Utu

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Naibu Waziri Masauni amesema ni lazima wananchi washirikiane na vyombo vya ulinzi na usalama kufichua wahamiaji haramu wanaoishi maeneo mbalimbali nchini.

“Serikali ya Tanzania inaheshimu haki za kila mtu na ndio maana tumeingia mikataba mbalimbali ya kimataifa yenye kulinda utu wa kila raia awe raia au mgeni aliyepo nchini, lakini hatutokuwa tayari kuona wahamiaji wasiofuata sheria za nchi wakiingia nchini kinyume na  taratibu zilizowekwa,” alisema Masauni

“…. Nawasihi wananchi watoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kufichua wageni wanaoingia nchini kinyume na utaratibu kwani wakiwaacha wanaweza kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini.” Aliongeza Masauni.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala amesema Idara yake itaendelea kutumia teknolojia katika kuendesha shughuli za uhamiaji lengo ikiwa kudhibiti uhalifu na kuiongezea mapato serikali huku akiahidi kuzuia na kudhibiti wahamiaji wanaoingia nchini kinyume na taratibu

Siku ya Maadhimisho ya Wahamaji Duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo Disemba 18 huku Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni “Uhamiaji Unaozingatia Utu”
 Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Mhandisi  Hamad Masauni, akisikiliza  maelezo  juu  ya  historia  ya  mabadiliko  ya  Pasi za Kusafiria  kutoka kwa mtaalamu wa pasi hizo,  Sajini  wa  Uhamiaji, Vedasto  Rweikiza(kulia), wakati  wa  Maadhimisho  ya  Siku  ya  Kimataifa  ya  Wahamiaji  Duniani, ambayo  kwa  hapa  nchini  yamefanyika  leo, katika  Viwanja  vya  Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli  mbiu  ikiwa  Uhamiaji  Unaozingatia Utu. Kushoto ni Kamishna Jenerali  wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Mhandisi  Hamad Masauni, akipokea zawadi  kutoka  kwa  Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Salma Panja(kulia),  baada ya kutembelea mabanda ya maonyesho  wakati wa Maadhimisho  ya  Siku  ya  Kimataifa  ya  Wahamiaji  Duniani, ambayo  kwa  hapa  nchini  yamefanyika  leo, katika  Viwanja  vya  Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kauli  mbiu  ikiwa  Uhamiaji  Unaozingatia Utu. Kushoto ni Kamishna Jenerali  wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala.
 Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Mhandisi  Hamad Masauni na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala (kushoto), wakiangalia pasi ya kusafiria walipotembelea mabanda ya maonyesho wakati  wa  Maadhimisho  ya  Siku  ya  Kimataifa  ya  Wahamiaji  Duniani, ambayo  kwa  hapa  nchini  yamefamyika  leo, katika  Viwanja  vya  Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli  mbiu  ikiwa  Uhamiaji  Unaozingatia Utu.
 Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Mhandisi  Hamad Masauni, akizungumza wakati  wa  Maadhimisho  ya  Siku  ya  Kimataifa  ya  Wahamiaji  Duniani, ambayo  kwa  hapa  nchini  yamefamyika  leo, katika  Viwanja  vya  Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli  mbiu  ikiwa  Uhamiaji  Unaozingatia Utu.
Kamishna Jenerali  wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, akizungumza wakati  wa  Maadhimisho  ya  Siku  ya  Kimataifa  ya  Wahamiaji  Duniani, ambayo  kwa  hapa  nchini  yamefanyika  leo, katika  Viwanja  vya  Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli  mbiu  ikiwa  Uhamiaji  Unaozingatia Utu..Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA), Dkt. Anold Kihaule, akisikiliza  maelezo  kutoka kwa mtaalamu wa pasi za kusafiria,  Sajini  wa  Uhamiaji, Vedasto  Rweikiza (kulia), wakati  wa  Maadhimisho  ya  Siku  ya  Kimataifa  ya  Wahamiaji  Duniani, ambayo  kwa  hapa  nchini  yamefanyika  leo, katika  Viwanja  vya  Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli  mbiu  ikiwa  Uhamiaji  Unaozingatia Utu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad