HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 17, 2018

TBL YANG'ARA TENA TUZO YA MWAJIRI BORA 2018

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imepata tuzo kutoka Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) ya utekelezaji vigezo vya Raslimali Watu kwa viwango vya juu, katika hafla ya kutunukia Waajiri bora nchini iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Sera , Bunge ,Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Mh.Jenesta Mhagama.

Mbali na tuzo hiyo,TBL ambayo hivi karibuni ilishinda tuzo ya kimataifa inayotolewa na taasisi ya Top Employers Institute ya nchini Uholanzi, ilipata tuzo ya ATE katika kipengele cha kutoa mafunzo na kuendeleza wafanyakazi wake.

Akizungumzia ushindi huo,Mkurugenzi Raslimali Watu wa TBL,David Magese alisema “Ushindi wa tuzo hii umechangiwa na timu nzuri ya wafanyakazi wa kampuni ,Wafanyakazi wote wa TBL tunashirikiana kufanya kazi kwa bidii na malengo ya kuifanya kampuni kuwa sehemu ambayo inavutia watu kufanya nayo kazi,na hii ni ndoto yetu kubwa katika maeneo yote barani Afrika ambapo kampuni inafanyia biashara zake”.Alisema.

Magese aliongeza kusema kuwa kampuni ya TBL imewekeza kwa wafanyakazi wake na inazo programu malimbali za mafunzo ya kuendeleza taaluma na ujuzi wao ,ukuzaji vipaji vya wafanyakazi na mpango wa kuwaandaa viongozi wa kampuni wa siku za mbele unaojulikana kama Global Management Trainee (GMT) unaosimamiwa na kampuni yake mama ya ABInBev.

Alisema tuzo mbalimbali ambazo kampuni ya TBL imekuwa ikitunukiwa na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi zinadhihirisha dhamira ya kampuni ya kufanikisha kuchangia kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini kupitia uwekezaji wake sambamba na kufanikisha mkakati wa Serikali wa Tanzania ya viwanda.

Ikiwa kampuni kubwa ya kutengeneza bia nchini,TBL imekuwa mstari wambele kuhakikisha inazalisha bidhaa zenye ubora unaokubalika kimatifa sambamba na kuhakikisha inatumia malighafi za ndani,mpango ambao pia unawanufaisha wakulima na wafanyabiashara wa kitanzania wanaoiuzia kampuni malighafi.
Meneja ukuzaji wa Vipaji wa TBL ,Lilian Makau ( Kushoto) akipokea tuzo kwa niaba ya kampuni kutoka kwa Waziri wa Sera , Bunge ,Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu, Mh. Jenesta Mhagama baada ya kampuni kuibuka kidedea kwa kushika nafasi ya pili katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City mwishoni mwa wiki, Kulia ni Naibu waziri wa wizara hiyo , Anthony Mavunde.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group, wakifurahia ushindi wa mshindi wa pili wa tuzo za mwajiri bora 2018.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad