HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 18, 2018

TAEC YAFUNGA VITUO 69 VYA AFYA TANZANIA BARA


Na Vero Ignatus, Arusha
Tume ya nguvu za Atomic Tanzania (TAEC) imefungia vituo 69 vya afya Tanzania bara kwa kutotimiza vigezo vya kuendesha vituo hivyo

Hayo yameelezwa na kaimu mkurugenzi wa tume ya nguvu za atomic Tanzania Dkt. Wilbard Muhogorawakati akifungua mafunzo hayo ya kitaifa ya kinga ya mionzi kwenye uchunguzi wa magojwa kwa madaktari kutoka Tanzania bara ambayo yamefanyika jijini Arusha

Amesema sheria ya nguvu za atomic inatoa vipengele ambavyo vinataka mafunzo kwa wafanyakazi wote waliopo kwenye sehemu ya mionzi yaweze kufanyika kwa kuwa kinga ya mionzi itatolewa kwa watu wote

"Mpaka sasa tumefungia vituo 69 kwa kutokuwa na leseni na mafunzo kwa wafanyakazi wanaotumia vipimo vya diology, na kutokuwa na ubora wa maamshine na majengo hiyo ndo sababu iliyofanya tukafungia vituo hivyo" alisema Dkt. Wilbard

Amewataka waajiri kuwapeleka wafanyakazi wao kwenye mafunzo ya kinga ya mionzi ili kuweza kupata elimu na hiyo imewekwa kila baada ya miezi mitatu kwa kila mkoa

Kwa upande wake Bakari Msongamwanja kutoka taasisi ya mifipa na mishipa ya fahamu Moi amesema umuhimu wa mafunzo hayo yatawasaidia kujua umuhimu wa kumlinda mgonjwa na waliowazunguka na kupitia elimu hiyo watawalinda wagonjwa Aidha amesema kupitia mafunzo hayo ataenda kuisaidia jamii hasa katika kutoa elimu kwa jamii na kupunguza changamoto zinazotokana na madhara ya mionzi

Kelvini James ni mmoja wa mshiriki ambaye ametokea hospital ya Ikonda amesema umuhimu wa mafunzo hayo yatasaidia kuwalinda wao kujikinga na madhara ya mionzi ambapo changamoto ambayo imekuwepo ni wagonjwa wanaokwenda hospitali kutokujua namna ya kujikinga na mionzi

Hata hivyo amewataka waajiri kutimiza wajibu hasa kwa wafanyakazi kuwa na elimu ya kinga ya mionzi ambayo imekuwa ni changamoto kubwa kwa baadhi ya vituo vya afya hapa nchini. Hata hivyo mafunzo hayo ni kwa ajili ya vituo vya afya na yataendelea kufanyia na watu wa migodini na viwandani pamoja na kufanya ukaguzi maeneo mbalimali hapa nchini

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad