HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 5 December 2018

OFFICIAL LYN ASEMA AMEKUJA KIVINGINE KWENYE BONGOFLEVA

MSANII wa michezo ya mrembo husika wa Kwenye wimbo (VIDEO QUEEN) Irene maarufu kama official Lyn  aingia rasmi Kwenye tasnia ya muziki wa Bongofleva.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam Lyn ambae alianza kujulikana Kwenye video ya Msanii Rayvan Kwenye kibao chake cha kwetu alishirikishwa kama video queen amesema rasmi ameingia Kwenye muziki akiwa tayari ameshafanya wimbo unaokwenda kwa jina la Chafu ambao umetoka Leo .

Kisheria natambulika na Baraza la Sanaa  (BASATA) nikiwa kama Muimbaji pia ni Msanii hivyo basi  niwatoe hofu mashabiki zangu alisema Lyn.

Hata hivyo ameeleza utofauti wake na video queen wengine ambao wameshaingia Kwenye tasnia ya muziki kuwa atanyanyua vipaji vya queen video chipukizi na kuwa nafasi kuonekana Kwenye baadhi ya kazi zake za muziki atakazokuwa anafanya kuanzia sasa kwani hata yeye alitokea huko huko na baadae kujulikana.

Hata hivyo Lyn amesema kuwa anaomba mashabiki wake wampokee kwa mikono yote kama walivompokea wakati akiwa video queen ambapo kwa sasa hatoweza kurudi Kwenye kazi hiyo ya zamani.

Pia ametolea ufafanuzi kuhusu wimbo wake mpya wa chafu ambao amefanya Kwenye studio za Black na video amefanya na director hascana nchini south Africa huku Mashairi akitungiwa na Msanii Marioo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad