HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 31 December 2018

NITAWAPUMZISHA WACHEZAJI WANGU KUNA MAKOMBE MUHIMU- ZAHERA MWINYI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KUELEKEA katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameweka msimamo wa kuwapumzisha wachezaji wake muhimu wa kikosi cha kwanza. Zahera  amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya Klabu hiyo Jangwani  Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuelekea mashindano hayo,  atawapumzisha wachezaji baadhi ya wachezaji wake kutokana na kukabiliwa na mashindano mengi msimu huu. Zahera ameeleza kuwa kufuatana na uwepo wa mashindano hayo ni vema wakawapumzisha wachezaji kadhaa kwa ajili ya kuweka nguvu katika Ligi Kuu Bara.

"Kufuatana na nguvu yetu tulionayo (wachezaji) inatubidi tuangalie wapi tutapata faida, tupo na ligi kuu, tupo na Azam federation cup , Mapinduzi Cup na Sport Pesa. "Inabidi sisi kama Yanga tuwe na malengo kwenye kitu chenye manufaa kwetu tukiamua kuyataka makombe yote tunaweza kosa yote ivyo lazima baadhi ya wachezaji wapumzike kwaajili ya ligi na ASFC", amesema Zahera.

Mbali na hilo Zahera amefanya Kikao na wachezaji wa zamani wa Klabu hiyo kongwe na kumpongeza kwa jitihada kubwa anazozifanya za kuisaidia timu ingawa ipo katika kipindi kigumu.
Akizungumza kwa niaba ya wengine Mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga Sunday Manara 'Computer'  amesema kuwa  wanampongeza Kocha na benchi zima la  ufundi na wako pamoja nao.

Sunday manara amesema akiwa kama mwanayanga na mchezaji wa zamani wa timu hiyo wanaendelea kuunga mkono jitihada zote zinazofanywa na Wachezaji wa timu yao wakiongozwa na kocha Zahera. Mbali na hilo Manara amesema mpaka sasa yanga itaendelea kufanga vizuri kulingana na mikakati thabiiti inayofanywa na uongozi wa timu hiyo.
Kocha Mkuu wa Yanga Zahera Mwinyi (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Dismas Ten.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad