HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 16 December 2018

MUST YATIMIZA MAAFALI YA 6 KWA MWAKA HUU 2018..


Spika mstaafu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzanian Mhe.Pius Msekwa ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Sayansi  na Teknolojia Mbeya akitoa Hotuba katika siku ya mahafali  ya sita  ya Chuo  cha  Sayansi na Teknolojia Mbeya.Mhe.Msekwa Aliwatunuku madaraja mbalimbali wahitimu waliofanikiwa kufuzu masomo katika nyanja mbalimbali za madaraja ikiwemo, Shahada, Stashahada nakozi mbalimbali zitolewazo na chuo hicho cha Sayansi na Teknolojia kilichopo mkoani Mbeya. Hii ni Mahafali ya 6 ya chuo hicho tangu kuanzishwa kwake ambapo Mhe.Pius Msekwa alitoa pongezi kwa uongozi wachuo ikiwemo watendaji wote wa chuo hicho pamoja na kuwaasa wahitimu kuwa na maadili mema na yaliyotukuka huko waendapo.
Mhe.Zakia  Meghji  ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Chuo Cha Sayansi  na Teknolojia,Mbeya( MUST) akisoma risala mbele ya mgeni rasmi katika siku ya  mahafali ya sita ya Chuo Cha Sayansi na Teknolojia Mbeya
Prof.Joseph Msambichaka,Makamu, mkuu wa Chuo cha Sayansi na  Teknolojia Mbeya akisoma risala iliyoandaliwa kwa ajili ya mgeni rasmi  siku ya mahafali ya sita ya Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya.
Katika taswira ni baadhi ya wahitimu  wakivaa kofia baada ya Kutunukiwa daraja husika katika siku ya mahafali ya sita ya Chuo cha Sayansi na Teknolojia  MbeyaNo comments:

Post a comment

Post Bottom Ad