HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 22, 2018

MGOMBEA WA CHAMA CHA MAPINDUZI APITA BILA KUPINGWA

MGOMBEA Udiwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi katika kata ya Utiri  wilaya ya Mbinga Aidan Nombo, amepita bila kupingwa kufuatia wagombea wa vyama vingine kushindwa kushiriki katika kinyang’anyiro hicho. Nombo ambaye  alikuwa diwani wa kata hiyo  kwa tiketi ya Chadema kuanzia mwaka 2015 hadi Oktoba 2018 alipojivua uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM alikuwa mgombee pekee  ambaye alijitokeza kuomba  kugombea nafasi hiyo.

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mbinga mjini ambaye pia mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Mbinga Grace Quintine alisema, kwa mamlaka aliyonayo kama msimamizi wa uchaguzi amemteua mgombea  wa CCM kuwa diwani wa kata ya Utiri. Alisema, kwa mujibu wa kifungu cha 45(2) cha sheria za uchaguzi za serikali za mitaa cha mwaka 1979 sura ya 292 amelazimika kumteua Aidan Nombo wa CCM kuwa diwani baada ya kupita bila kupingwa wakati taratibu za kumtangaza rasmi zikisubiriwa kufanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo  ndiyo yenye mamlaka ya kufanya hivyo.

Kwa upande wake Nombo alisema, ushindi huo alioupata bila kupingwa ni ishara tosha kuwa Chama cha Mapinduzi kimekubali  sana kwa watanzania na ndiyo sababu inayopelekea hata wagombea wake wa nafasi mbalimbali kushinda kwa kura nyingi na wengine kupuita bila kupingwa. Alisema,   mara atakapoanza majukumu yake,kipaumbele cha kwanza ni kukamilisha miradi ya maendeleo ili iweze kuwasaidia wananchi wa kata ya Utiri kupata muda mwingi wa kushiriki katika kazi za kiuchumi.

Aidha, amewaomba wanachama wa Chama cha Mapinduzi kumpa ushirikiano na kuhaidi kuwa ataendelea kuwa mtiifu na mwaminifu kwa chama chake na viongozi ili kwa pamoja waweze kutekeleza Ilani ya Chama ambayo imedhamiria kuondoa kero na changamoto kwa Watanzania.

Alisema, awali alilazimika kujivua uanachama wa Chadema na na hivyo kupoteza nafasi ya udiwani kupitia chama hicho kujiunga na ccm baada ya kuona viongozi wa Chadema wanakifanya Chama kama mali yao binafsi na kuwataka wanachama wengine kutopoteza muda wao  ndani ya Chama.
Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Mbinga mjini ambaye pia ni mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma Grace Quintine kushoto akikabidhi cheti cha ushindi kwa diwani wa kata ya Utiri kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Aidan Nombo ambaye alipita bila kupingwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad