HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 22 December 2018

DC Chongolo azinduwa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (katikati) akionesha bango kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya hiyo usiku huu. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation, Bw. Ally Mbega wakishiriki. Kampeni hiyo naendeshwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (wa pili kulia) akionesha bango kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya hiyo usiku huu. Wengine ni viongozi waandamizi wa Shirika la TTCL wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (wa tatu kulia). Kampeni hiyo naendeshwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya hiyo usiku huu.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya hiyo usiku huu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba akizungumza katika kampeni hizo zilizofanyika katika Uwanja wa CCM Mwinjuma.
Burudani kabambe kutoka kwa madansa zikiendelea.
Msanii Shilole akiwapagawisha washiriki katika kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga ya Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation.
Wasanii Shilole na Man Fongo (kulia) wakiwapagawisha washiriki katika kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga ya Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation.
Msanii Man Fongo akitoa burudani katika kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga ya Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation, katika Uwanja wa CCM Mwinjuma.
Meza kuu katika kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga ya Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation, katika Uwanja wa CCM Mwinjuma, wakishuhudia burudani za wasanii anuai.
Msanii Belle9 akitoa burudani katika kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga ya Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation, katika Uwanja wa CCM Mwinjuma.
Belle9 akitumbuiza katika kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga ya Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation, katika Uwanja wa CCM Mwinjuma.

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo amezinduwa rasmi kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga inayoendeshwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation ikiwa ni kuhamasisha uzalendo kumuunga mkono Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kauli ya Juni 21, 2018 alipokuwa akipokea gawio la Tsh Bilioni moja na nusu kutoka TTCL Corporation.

Akizungumza DC Chongolo katika uzinduzi huo ulioenda sambamba na burudani toka kwa wasanii mbalimbali, aliwataka wana-Kinondoni kuwa wazalendo kwa kutumia huduma za TTCL ili kukuza uchumi wa Tanzania moja kwa moja kutokana na faida zinazopatikana. Alisema TTCL ni Shirika la umma na linapofanya vizuri kifaida Watanzania wenyewe ndio ufaidika tofauti na makampuni mengine yanayomilikiwa na watu wa nje ya nchi.

"...Mmesikia hivi karibuni Shirika hili lilitoa fedha shilingi bilioni moja na nusu na kuipa Serikali kama gawio, fedha hizi za Serikali hutumika kujenga miundombinu na shughuli zingine za maendeleo kwa Watanzania," alisema DC Chongolo.

Alisema kadri kampuni hii inavyofanya vizuri kifaida na jamii inanufaika hivyo kuwaomba wananchi kutumia bidhaa na huduma za TTCL Corporation ili isonge mbele zaidi.

Awali akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba alisema kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga imezunguka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Miji mashuhuri ikiwa ni kuunga mkono hamasa iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Magufuli siku ya tarehe 21 Juni 2018 alipokuwa akipokea gawio la Tsh Bilioni moja na nusu kutoka TTCL Corporation.

Katika Kampeni hizo jukwaa la burudani lilipambwa na wasanii mbalimbali maarufu, akiwemo Shilole, Man Fongo, Belle 9 pamoja na wasanii chipukizi na vikundi kabambe vya madansa.
Baadhi ya wananchi wakijisajili kutumia mtandao wa TTCL
Sehemu ya wananchi wakiwa katika kampeni hiyo.
Madansa wakikimbiza wapenzi wa TTCL.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad