HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 5 December 2018

BENKI YA I&M KUWAWEKA KARIBU WATEJA WAKE KATIKA MSIMU HUU WA SIKUKUU

Na Agness Francis, Globu ya Jamii
Benki ya I & M inaendelea kutoa zawadi kwa wateja wake katika droo  ya pili JIDABO na I & M bank chini ya usimamizi kutoka Bodi ya Taifa  ya Michezo ya Kubahatisha iliyochezeshwa leo ambapo washindi  watano wamepatikana kutoka sehemu mbali mbali hapa nchini 

Akizungumza na Waandishi wa  Habari leo Jijini Dar es  Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Wateja na reja reja, Ndabu Swere amesema kuwa  promosheni hiyo iliyoanza mwezi Octoba na kuendelea mpaka Disemba kwa kila mwezi kutaja washindi watano wa droo hiyo. 

Ndabu amesema washindi watano waliopatikana leo ni sehemu ya washindi 15 ambao watapatikana katika kipindi chote cha miezi mitatu ya promosheni ya "JIDABO na I&M". Aidha Ndabu amesema kuwa mpaka  sasa wameshapata jumla ya washindi 10 na kubakiza wengine  5 ambao watapatikana katika droo ya mwezi huu

"Ili kuweza kushiriki Promosheni hii mteja anapaswa afungue akaunti ya Akiba, biashara, mtoto katika tawi lolote la Benki ya I & M katika kipindi chote cha promosheni, kwa mteja ambaye tayari ana Akaunti ya Benki hiyo anapaswa kuhakikisha kuwa ana akiba ya kiasi cha fedha  shilingi 200000, akiwa anamiliki akaunti ya biashara, au 100000, Ikiwa anamiliki Akaunti nyingine zinazohusika katika promosheni," amesema Ndabu.
 Mkuu wa kitengo cha Wateja wa reja reja wa Benki ya I & M Ndabu Lilian Swere akiwataja washindi watano wa droo ya pili ya Promosheni ya JIDABO na I& M Bank iliyochezwa leo Jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko na Mawasiliano Emmanuel Kiondo, Benki ya I & M akiwa na mmoja ya mfanyakazi wa Benki hiyo wakichezesha droo ya pili iliyofanyika leo na kuwatangaza washindi  watano wa Promoshei ya JIDABO na I & M Bank chini ya usimamizi kutoka bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad