HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 15, 2018

WAZIRI KIGWANGALLA AITEGA BODI YA WADHAMINI YA TaFF

Na Lusungu Helela-Dodoma
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameiagiza Bodi ya pili ya Wadhamini ya Mfuko  wa Misitu Tanzania (TaFF) isimamie utekelezaji wa uanzishwaji wa  mradi wa viwanda  vya kusindika, kuchakata  na kufungasha asali katika mikoa inayofuga nyuki ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kujenga uchumi wa viwanda

Waziri Kigwangalla ametoa agizo hilo   wakati alipokuwa akizindua  Bodi ya pili ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania uliofanyika leo jijini Dodoma.

Kufuatia agizo hilo, Waziri Kigwangalla ameiambia Bodi hiyo kuwa pamoja  na utekelezaji wa maagizo mengine aliyowapatia, suala la uanzishwaji viwanda vya kusindika, kuchakata na kufungasha asali na bidhaa nyingine zitokanazo na ufugaji nyuki katika mikoa ya Tabora, Kigoma, Katavi, Rukwa, Songwe na Mbeya liinapaswa kupewa uzito wa  juu kiutekelezaji.

Waziri Kigwangala ameongeza kuwa ni azma ya Serikali ya awamu ya tano kuifikisha Tanzania katika uchumi wa  kati ifikapo 2025 na kuwa suala hilo lina  umuhimu mkubwa  kwa wafugaji wa nyuki na uhifadhi mazingira..

Ameongeza kuwa endapo suala hilo la viwanda litafanikiwa , itasaida  kuchochea jamii  kuwa mstari wa mbele  kulinda misitu badala ya sasa jamii kujikita kwenye ukataji  miti ovyo hali inayotishia nchi kugeuka kuwa  jangwa kama hatua za haraka hazitachukuliwa. 

Amesema kiwango cha  ufugaji nyuki kwa mikoa inayofuga  si cha kuridhisha kwa vile wafugaji walio wengi  wamekuwa wakifuga kwa mazoea jambo ambalo wafugaji walio wengi kuamua kuachana na shughuli hiyo na kugeukia uchomaji mkaa pamoja na kujiingiza kwenye   shughuli za uharibifu mazingira.

Waziri Kigwangalla amesema uanzishwaji wa viwanda hivyo vitasaidia jamii kuwa na  kipato mbadala hali itakayopelekea wananchi  kuanza kuona umuhimu wa kulinda na kuhifadhi misitu.

"Mkianza kuwekeza upande wa magharibi  ambapo kuna zaidi ya asilimia 60 ya misitu yote hapa nchini wananchi, wakiwemo Nzega, Sikonge, Uyui, Tanganyika, Mlele, Mpanda na Kaliua hawatakubali kuona mtu au kikundi cha watu kinaharibu misitu.

 "Nataka kuona mapinduzi makubwa kwenye ufugaji nyuki kwa kuiwezesha jamii  kuwa na  mizinga ya kisasa ili iweze kufuga nyuki  kisasa na hatimaye wapeleke kwenye viwanda wakajifunze kufungasha kisasa, ili ipate bei kubwa, na mwisho wa siku wataona faida ya kuwa na misitu.


Wakati huo huo, Waziri Kigwangalla ameitaka Bodi hiyo isimamie utekelezaji wa uhuishaji wa misitu ya kijiji pamoja na ile ya Halmashauri ambayo tayari imeharibiwa kwa kuanza kupanda miti ya  asili pamoja na kuanzisha mashamba mapya ya miti.

Naye, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu ameitaka Bodi hiyo isimamie utekelezaji wa upandaji miti kwa vile mikoa kama Shinyanga hali ya uharibifu misitu inatisha,

Ameongeza kuwa kama hatua za makusudi hazitachukuliwa itafika kipidi ambacho akina mama wa vijijjini watakuwa wakitembea umbali wa kilomita 200 kwa ajili yua kutafuta kuni

Awali, Kaimu Katibu ,Mkuu wa Wizara hiyo, Lucius Mwenda amesema tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo umekuwa ukisaidia sana kwenye uhifadhi licha ya kuwa mfuko huo umekuwa na changamoto ya uhaba wa watumishi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. Romanus Ishengoma amemhakikishia Waziri Kigwangalla kuwa Wajumbe wa Bodi watafanya kazi kwa weledi na utaalamu wa hali ya juu na kuanza na suala la uanzishwaji wa viwanda vitavyowasaidia wafugaji nyuki nchini.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza  na Wajumbe wa  Bodi ya pili ya Wadhamini  ya Mfuko wa Misitu Tanzania  pamoja na sekretarieti ya Bodi hiyo wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika jijini Dodoma. 
 Mwenyekiti wa  Bodi ya pili ya Wadhamini  ya Mfuko wa Misitu Tanzania, Prof. Romanus Ishengoma akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Romanus Ishengoma  mara baada ya Waziri Kigwangalla  kuzindua  Bodi hiyo jijini Dodoma.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo,  Mhe. Constantine Kanyasu ( kushoto)  wakimkabidhi kabrasha Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania,  Prof. Romanus Ishengoma (kulia) ikiwa ni ishara ya kumkabidhi majukumu ya kuusimamia Mfuko huo wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika leo jijini Dodoma.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo,  Mhe. Constantine Kanyasu (kushoto)  wakimkabidhi kabrasha Mjumbe  wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa  (kulia) ambaye pia  ni Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki  wakati  Waziri Kigwangalla alipokuwa akizindua wa Bodi hiyo jijini Dodoma. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo,  Mhe. Constantine Kanyasu (kushoto)  wakimkabidhi kabrasha Mjumbe  wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania, Tuli Msuya (kulia)  wakati  Waziri Kigwangalla alipokuwa akizindua wa Bodi hiyo jijini Dodoma
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo,  Mhe. Constantine Kanyasu (kushoto)  wakimkabidhi kabrasha Mjumbe  wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania, Prof, Dos Santos Silayo (kulia) ambaye pia  ni Mtendaji  Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)  wakati  Waziri Kigwangalla alipokuwa akizindua wa Bodi hiyo jijini Dodoma. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa  Bodi ya pili ya Wadhamini  ya Mfuko wa Misitu Tanzania  pamoja na sekretarieti ya Bodi hiyo wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika jijini Dodoma. Wengine ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu(wa tatu kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Romanus Ishengoma (wa tatu kulia). 
                     ( Picha zote na  Lusungu Helela-MNRT) 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad