Katika mkataba huo StarTimes
itasaidia programu mbalimbali za SOS Children’s Village katika Mikoa zaidi ya
saba ikiwemo Unguja, Pemba, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Iringa na Mufindi
na program hizo zitalenga hasa kwenye kupanua nafasi za kujifunza na kukuza
uzoefu miongoni mwa Vijana wa SOS Children’s Village.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa makubaliano hayo mwanasheria mkuu wa Star Media (T) Ltd Justine Ndege amesema kuwa kwa vijana waliopo, kazi yao ya kwanza sio kuwa na uhuru. Kwao jambo la msingi kwanza ni kuishi tofauti ya maisha huru yenye heshima na maisha yenye misukosuko na mahangaiko ndicho wanacholenga kukabiliana nacho.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa makubaliano hayo mwanasheria mkuu wa Star Media (T) Ltd Justine Ndege amesema kuwa kwa vijana waliopo, kazi yao ya kwanza sio kuwa na uhuru. Kwao jambo la msingi kwanza ni kuishi tofauti ya maisha huru yenye heshima na maisha yenye misukosuko na mahangaiko ndicho wanacholenga kukabiliana nacho.
Ndege amesema kuwa, Ushirikiano baina ya
kampuni Startimes na SOS Village utapiga hatua katika
kuwapeleka Vijana katika soko la ajira na kuwapatia namna au njia za
kujitengenezea kesho yenye uimara na uhakika zaidi katika jamii zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa SOS Childre’s
Village Dvid Mulongo amesema kuwa moja ya mambo ambao StarTimes itafanya ni
kuwapatia nafasi vijana kutoka SOS Villages Tanzania bara na Zanzibar kujifunza
kwa vitendo kazi mbalimbali zilizopo kwenye kampuni yao, ushauri, mafunzo ya
kiufundi kuhusu namna ambavyo StarTimes inafanya kazi hasa katika Idara ya
Masoko na kuhusu bidhaa zake ili kukuza uelewa wa kazi na ajira kwa Vijana.
Mulongo amesema kuwa
kampuni ya Star Media (T) Ltd itatumia akaunti zake za mitandao ya kijamii
kuzungumzia juu ya programu za SOS Village ikiwa ni moja ya mambo ambayo
yatafanywa chini ya ushirikiano huo ambao ni nafasi ya kipekee kwa Vijana kukua
na kuendeleza kiuchumi.
Barani Afrika, watu
milioni 200 wana umri kati ya miaka 15 na 24 ikiwa ni zaidi ya asilimia 20 ya
watu wote kwa bara zima. Idadi inazidi kuongezeka kwa kasi, na itaongeza presha
katika upatikanaji wa nafasi za kazi. Katika hii, Vijana ni 37% ya watu
wanaofanya kazi, lakini bado Vijana ni 60% ya watu wasio na ajira. Nchini
Tanzania kwa watu wanaoweza kufanya kazi (miaka 15 - 64) ni 23,466,616 ambayo
ni sawa na 52.2% ya watu wote; Vijana (miaka 15 – 35) ni 15,587,621 sawa na
66.4% ya watu wanaoweza kufanya kazi.
Kwa ushirikiano huo wa
StarTimes na SOS Children’s Village utasaidia kwa kiasi kikubwa kutengeneza Vijana
ambao wataweza kuingia katika soko la ajira ili kupunguza kwa kiasi kikubwa
tatizo la ukosefu wa ajira.
Mwanasheria Mkuu Star Media (T) Ltd, Justine Ndege(kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa kuingia makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kusaidia familia na watoto/Vijana wanaoishi katika changamoto ya mazingira hatarishi. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa SOS Children's Village, David Mulongo
Mwanasheria Mkuu Star Media (T) Ltd, Justine Ndege(kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa SOS Children's Village, David Mulongo(kushoto) wakisaini makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kusaidia familia na watoto/Vijana wanaoishi katika changamoto ya mazingira hatarishi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa ofisi za SOS Children’s Villages Tanzania jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria Mkuu Star Media (T) Ltd, Justine Ndege(kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa SOS Children's Village, David Mulongo(kushoto) wakipeana mikono mara baada ya kumaliza kuingia makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kusaidia familia na watoto/Vijana wanaoishi katika changamoto ya mazingira hatarishi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa ofisi za SOS Children’s Villages Tanzania jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja
No comments:
Post a Comment