HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 28 November 2018

SHIRIKA LA UMOJA WA WA MATAIFA WAANDAA MKAKATI WA KITAIFA WA KUSIMAMIA TAKA NCHINI.

   Na.Khadija Seif, Globu ya jamii
  SHIRIKA la umoja wa mataifa linalojishugulisha na mazingira (AGENDA) limezitaka nchi zilizopo katika Ukanda wa Jangwa la Sahara kutunga sera zakusimamia ukusanyaji wa taka Ngumu ili kulinda afya ya mazingira.


Wito huo umetolewa Leo jijini Dar es salaam katika mkutano wapili wa wadau wa kuandaa mkakati wa kitaifa wakusimamia taka Tanzania(AGENDA) ambapo  imewashirikisha Taasisi ,Wizara na Mamlaka mbalimbali za serikali,Makampuni binafsi na wawakilishi wa asasi za kirai.

Akizungumza na wanahabari Kiongozi wa shirika hilo kwa Ukanda wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara Prof. Abdrahman Bary amesema kushindwa kuhifadhi Takataka kumeleta madhara mengi kwa nchi zinazoendelea na kwa sasa mapambano yanaendelea katika kudhibiti uzalishaji wa taka. 

Aidha Bary ameeleza kuwa usimamizi bora wa taka ngumu ni muhimu kwa afya ya jamii,usalama na Mazingira bora kwa ujumla.

Hata hivyo amefafanua kuwa baadhi ya matatizo yanayolikabili jiji la Dar es salaam ni pamoja na ongezeko la kiwango cha juu cha idadi ya watu pamoja na uwezo mdogo kifedha wa kudhibiti taka.

Kwa upande wa Msimamizi wa mradi kudhibiti takataka ngumu Prof. Jamidu Katima kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam amesema linakadiriwa kuzalisha tani 4600 za taka kwa siku huku taka nyingi zikiwa hazipelekwi sehemu za kuhifadhia takataka (dampo) hivyo kuhimiza mamlaka husika kusimamia taratibu za uhifadhi, Kusafirisha na kutupa taka ili kulinda mazingira

Katima amesema mkakati huo unalenga kuona nchi zinazoendelea zinapambana katika kudhibiti taka Ngumu pamoja na uzalishaji wa taka Ngumu, kutumia taka kama vyanzo vya uzalishaji mbolea, taka zinazoweza kurejelewa zirejelewe huku wakizalisha Ajira kwa vijana wao kupitia uhifadhi taka wakisasa.

Vilevile Katima amewapongeza shirika la Mazingira UN kutupatia Msaada wa kifedha kuwezesha uandaaji wa mkakati wa kusimamia taka.
 Msimamizi wa mradi kudhibiti takataka ngumu Prof. Jamidu Katima kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam akizungumza na wanahabari Jijini Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa pili wa wadau wa Kuandaa mkakati wa kusimamia Takataka
Washiriki katika Mkutano wa pili wa wadau wa Kuandaa mkakati wa Kitaifa wa kusimamia Taka nchini uliofanyika jijini Dar es salaam ulioandaliwa na Shirika la kudhibiti na kusimamia Taka (AGENDA) 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad