HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 13, 2018

RAYVANNY AWAJIBU BASATA KIAINA KUHUSU WIMBO WAKE KUFUNGIWA


Na Khadija Seif,Globu ya jamii
MSANII aliyekuwa kwenye ubora wake kwenye muziki wa kizazi kipya maarufu Bongo Fleva kutoka lebo ya WCB Raymond Mwakyusa a.k.a Rayvanny ameamua kuonesha hisia zake baada ya wimbo wake wa Mwanza kufungiwa.

Rayvanny kupitia ukurasa wake wa Instagramu amesema amesikitishwa na kitendo BASATA kuufungiwa  kwa wimbo huo ambao ameshirikisha Naseeb Abdul ‘Daimond Platinum’ kwa kile kilichodaiwa kuwa ni wimbo unaohamasisha ngono na ni kinyume cha maadili ya Kitanzania .

Rayvanny amesema kuwa taarifa za kufungiwa kwa wimbo wake amezipata lakini ni bora akaeleza machache .
Amesema Sanaa ni neno lililotokana na lugha ya kiarab lenye maana na ni ufundi anaotumia mwanadam kuwasilisha fikra au mawazo yake ndani ya fikra zake.

“  Sanaa ni nzuri, unajiona katika umbo lililosanifiwa ,kusanifu ni kuimba na kufanya kitu kwa kutumia usafi ili kuvutia watu kwa uzuri wake.Hivyo kazi yoyote ya sanaa inategemea uoneshe ufundi wa hali ya juu, ili iwe na mvuto kwa hadhira iliyokusudiwa.

Aidha amesema kuwa dhamira ya wimbo huo uliofungiwa haikua kutukana kama inavyoonekana sasa,ilikua ni kutoa burudani kwa hadhira iliokusudiwa ambao ni vijana.Pia ni  mafundisho ambayo kila siku serikali imekua ikipiga vita kama suala la Amber Ruti  kionjo kikisema " naogopa sentro michezo ya amber ruti ikiwa kwamba kijana yoyote anaesikiliza aogope kitendo hicho ataishia pabaya”

Sanjari na kipande kingine kinachosema "hapendagi mpasuo hataki shida BASATA ukiwa na maana kukataza mavazi mabaya au ya wazi ukiangalia yote hayo ni mafundisho ambayo msanii lazima uyafikishe katika lugha iliyosanifiwa.

“Lengo la kutumia neno Mwanza kutokana na siku chache zilizopita Mkoa huo ulikumbwa na maafa makubwa ajali ambayo ilisababisha vifo vya ndugu , jamaa na marafiki, hivyo basi tukaona ni vyema kuwafanyia mashabiki zetu wa Mwanza kitu kitakachowapa furaha ndio lilikuja wazo wa wimbo wa Mwanza,”amesema.

Pia amesema lakini wakaona usiende hivyo tu uwe na mafundisho ndani yake pamoja na burudani kwa vijana wa Mwanza na maeneo mengine na kwamba wimbo huo umepokelewa vizuri ikiwa ni ishara ya dhamira yao iliyokusudiwa imefanya kazi.
  
Aidha Rayvanny amesema kuna vyombo vya habari na sehemu mbalimbali miziki yao inaposikika yawezekana kukawa na Watoto pengine wimbo huu haikua hadhira tuliyoikusudia  hivyo kusikia kwao ikawa ni kinyume na maadili kwa sababu hadhira tuliyoikusudia  ni ya watu wazima miaka 18 na kuendelea ambao tunaamini ndio wanunuzi wa kazi zetu na ndio wahudhuriaji wa matamasha yetu.

Rayvan ametoa maoni na kusema swala la kufungia Wimbo huu kwa Vijana wenzetu ni kutunyima kufikisha ujumbe na burudani kwa hadhira yetu kwa njia ya sanaa mfano mitandao ya kijamii hakuna mtoto atakaeingia katika mitandao na hata kwenye tamasha la Wasafi Festival watakaokuja ni watu wazima ambao wimbo huu hauna madhara kwao Kwenye televisheni na redio na kuwaomba BASATA wakiwa kama wazazi au walezi kuwasaidia na kulitazama swala  kwani sanaa ni kazi ,ni ajira na ikiwa ni Ubunifu pia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad