HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 28 November 2018

Palozi wa Palestina Atembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

 Mkuu wa huduma za Sheria na Katibu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Maulid Kikondo akimwelezea Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli maendeleo ya ukarabati wa wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo alipofanya ziara katika taasisi hiyo na kutembelea ukarabati wa wodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam
  Baba wa mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua Hamis Daud akimwelezea Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli maendeleo ya mtoto wake baada ya kufanyiwa upasuaji huo alipofanya ziara katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kutembelea wagonjwa wodini leo Jijini Dar es Salaam
 Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akielezea namna wagonjwa wa moyo wanavyofanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na kupatiwa matibabu ya karibu katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) kwa balozi wa Palestina nchini  Mhe. Hamdi Mansour AbuAli alipotembelea chumba cha ICU wakati wa ziara yake katika taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam 
 Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli akizungumza na menejimenti ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) namna ambavyo Palestina itashirikiana na taasisi hiyo katika masuala mbalimbali ya afya ya moyo baada ya kufanya ziara kuangalia huduma zinazotolewa na taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiagana na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli baada ya kufanya ziara kuangalia huduma zinazotolewa na taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Pcha na: Genofeva Matemu - JKCI

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad