HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 27 November 2018

Naibu Waziri aomba wanaotumia ARVs kutoacha

 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko (kushoto) akibadilishana mawazo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF), Dk. Ellen Mkondya – Senkoro (kulia) wakati wa kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma. Katikati ni  Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng.
 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Uraghibishi na Habari wa TACAIDS, Jumanne Issango, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko pamoja na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng katika picha ya pamoja wakati wakisubiri kuwasili kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde kufungua kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. James Kiologwe (kulia) akimpokea Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye Hoteli ya Morena kufungua kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko.
 Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde mara baada ya kuwasili kwenye Hoteli ya Morena kufungua kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
 Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi ambaye pia ni Mbunge wa Biharamulo, Mhe. Oscar Mukasa pamoja Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na washiriki wa kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng akitoa salamu za UNAIDS wakati wa kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi ambaye pia ni Mbunge wa Biharamulo, Mhe. Oscar Mukasa akitoa salamu za kamati yake wakati wa kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. James Kiologwe akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Binilith Mahenge kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde kufungua kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
 Wadau mbalimbali wanaoshiriki kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
 Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng mara baada ya kufungua kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika 
Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng mara baada ya kufungua kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.

Na Mwandishi wetu, Dodoma
WATANZANIA wanaotumia dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi wametakiwa kuendelea kutumia pasipo kuacha, ili waweze kuishi maisha yenye afya iliyoimarika hivyo kuendelea kulitumikia taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde wakati akifungua kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
Alisema kati ya watu wanaoishi na VVU wenye umri wa miaka 15 hadi 64 ambao walitoa taarifa kuwa wanatumia dawa za kufubaza VVU, asilimia 87.7 ndio wamefubaza VVU ambapo wanawake ni asilimia 89.2 na wanaume ni asilimia 84.
“Napenda kuhamasisha watanzania wote wanaotumia dawa za kufubaza VVU waendelee kuzitumia pasipo kuchoka na kwa kufanya hivyo wataweza kuishi maisha yenye afya iliyoimarika na furaha na hivyo kuendelea kulitumia taifa vyema” alisema
Alisema kauli mbiu ya mwaka huu ni Pima VVU, Jitambue Ishi ambayo inaonesha ushahidi kutokana na matokeo ya utafiti wa viashiria vya UKIMWI wa mwaka 2016/2017 hapa nchini.
Alisema utafiti huo unaonesha kuwa kama nchi bado hatujafanya vizuri katika kutimiza malengo 90 ya kwanza ya kimataifa yaani asilimia 90 ya WAVIU nchini wawe wamepima na kujua hali zao ifikapo mwaka 2020.
Mavunde alisema matokeo yameonesha ni asilimia 52 tu ya WAVIU nchini wanajua hali zao.
“Hii ina maana kwenye eneo la kupima kuna vikwazo vingi vinavyowafanya watu hasa wanaume kutojua afya zao, pengine nchi bado hatujapata ufumbuzi bado kwani kutokana na matokeo ya utafiti huo ni asilimia 45 tu ya WAVIU wanaume wanajua hali zao” alisema
Alisema katika kutekeleza tisini ya pili yaani asilimia 90 ya WAVIU wajuao hali zao wawe wameanza dawa za ARV ifikapo mwaka 2020 kama nchi, imepiga hatua japo kwa kusuasua kidogo kwa upande wa wanaume.
Alisema utafiti wa mwaka 2016/2017 umeonesha kati ya watu wanaoishi na VVU wenye umri kati ya miaka 15 hadi 64 ambao wanajua hali zao za maambukizi asilimia 90.9 walianzishiwa dawa za kufubaza VVU, wanawake wakiwa asilimia 92.9 na wanaume ni asilimia 86.1.
Alisema serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika mapambano dhidi ya UKIMWI, inaahidi kutoa ushirikiano.
Alisema malengo hayo ni pamoja na kupunguza maambukizi mapya kwa asilimia 85 ifikapo mwaka 2023 kama ilivyobainishwa kwenye mkakati wa nne wa taifa wa kudhibiti UKIMWI nchini na hatimaye kufikia malengo ya sifuri tatu ifikapo mwaka 2030.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi  na Mwakilishi wa UNAIDS nchini, Dk. Leo Zekeng alisema Tanzania imepiga hatua kubwa kupambana na UKIMWI tangu miaka ya 1980 na kwa upatikanaji wa tiba tangu mwaka 2010 na misaada ya pamoja kutoka serikalini, mashirika ya kiraia yanayowakilisha watu wanaoishi na VVU pamojka na mashirika ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa.
“Tanzania inaweza kufikia lengo la kumaliza UKIMWI kama tishio la afya ya jamii kwa mwaka wa 2030 kama sehemu ya Malengo ya millennia na maono ya maendeleo ya Tanzania ya mwaka 2025” alisema
Alisema hadi sasa kwa bahati mbaya bado vikwazo vingine vya kupima VVU vinaendelea,
“Unyanyapaa na ubaguzi bado unaendelea huwazuia watu wasijaribu kuopima VVU na kujua hali zao, tunahitaji kukomesha unyanyapaa na ubaguzi katika mazingira yote hasa katika mazingira ya huduma za afya katika jamii yetu.” Alisema
Alisema upimaji wa siri wa VVU bado ni suala lenye wasiwasi, watu wengi bado hujaribu kupima baada ya kuwa na dalili za ugonjwa.
“Habari njema ni kwamba kuna njia nyingi za kuimarisha upatikanaji na upimaji wa VVU miongoni mwa wengine kuwa, kujipima, upimaji wa jamii husaidia watu kujua hali yao ya VVU” alisema
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko alisema kongamano hilo pia litaazimia mikakati mahususi itakayotoa matokeo zaidi katika kufanikisha dira ya kuwa na Tanzania isiyokuwa na UKIMWI kufikia mwaka 2030.
Alisema katika maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya UKIMWI duniani wamepanga kuzindua mkakati wa nne wa taifa wa kudhibiti UKIMWI (2018/2019- 2022/2023).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad