HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 19, 2018

BENKI YA AMANA WAZINDUA MIKOPO YA VIKUNDI KWA WAJASIRIAMALI WADOGO

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

BENKI ya Amana imeadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kuzindua rasmi mikopo ya vikundi ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kutimiza azma ya kuwafikia na kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dr Muslim Masoud amesema kuwa, mikopo hiyo ya vikundi itawawezesha wananchi wa kipato cha chini kujikwamua kiuchumi kama wanavyoendelea kuwawezesha wafanyabiashara wadogo kuwapa mikopo inayoanzia milioni moja hadi kumi.

Dr Masoud amesema kuwa, mpaka sasa wameshatoa mkopo wa Bilioni 143 kwa wateja wakubwa , wakati na wadogo na wakisaidia kuwainua kiuchumi wajasiriamali wengi na wafanyabiashara wadogo.

"Benki ya Amana inatimiza miaka saba na mpaka leo tumetoa mikopo ya Bilioni 143 kwa wateja wote wakiwa wameweza  kutimiza azma ya kuwafikia na kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini,"amesema Dr Masoud.

Amesema kwa wajasiriamali wadogo watatakiwa kuwa kwenye vikundi na sio mmoja mmoja nanwakiwa katika vikundi hivyo hawatahutajika kuweka dhamana ya aina yoyote.

Kwa upande wa Meneja wa Tawi la Benki ya Amana Barabara ya Nyerere, Aisha Awadh amesema, kwa sasa wanatoa mkopo huo kwa wajasiriamali wadogo wale wasio na ajira rasmi ikiwemo Mama Lishe, wauza bidhaa ndogondogo ila watatakiwa wajiunge kwenye kikundi kimoja ili wapatiwe mkopo huo.

Katika kuadhimisha miaka saba toka kuanzishwa kwa benki hiyo, wameweka ofa mbalimbali kwa wateja wao kupitia Wiki ya huduma kwa wateja kwa kupata punguzo maalumu la bei ya Viwanja vinavyotolewa kwa njia ya mkopo na benki hiyo, kwa kushirikiana na kampuni ya Property International Ltd ikiwemo na kuwaonesha viwanja mahali vilipo kwa kuwapeleka eneo husika.

Pia, katika kuwajali wateja wao wamezindua rasmi kampeni ya maalumu ya nufaika na akiba yako kwa wateja watakaowekwa kiasi kisichopungua milioni tano (5,000,000) kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu mfululizo watapata nafasi ya kushinda pikipiki aina ya TVS.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Amana, Dr Muslim Masoud  akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja pamoja na ofa mbalimbali walizojipanga kuzitoa kwa wateja wao katika kuadhimisha miaka saba toka kuanzishwa kwa benki hiyo.
 Meneja wa Tawi la Benki ya Amana Barabara ya Nyerere, Aisha Awadh  akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa mkopo wa vikundi kwa wajasiriamali wadogo utakaokuwa unatolewa kwneye tawi la benki hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Amana, Dr Muslim Masoud  akimsikiliza mteja wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja uliofanyika Tawi la Benki ya Amana Barabara ya Nyerere.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad