HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 3 October 2018

WANANCHI NAMBINDA WAMUOMBA MGOMBEA UBUNGE CCM KUTATUA KERO YA MKUNGA

Wakazi wa kijiji cha Nambinda Halmashauri ya wilaya ya Liwale Mkoani Lindi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mkunga katika zahanati ya eneo hilo hali ambayo inapelekea kina mama kutafuta wakunga wa jadi ili kupata huduma hiyo.

Wakizungumza na michuzi Blog wakati wa Kampeni za uchaguzi mdogo wa marudio ya nafasi ya ubunge katika jimbo la liwale wakazi wa kijiji hicho wamemuomba mgombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Zuberi Kuchauka kushirikiana na serikali kupata ufumbuzi wa changamoto hizo baada ya kupata ridhaa ya kuwatumikia wakazi hao.

Wakimnadi mgombea huyo katika kampeni za uchaguzi huo baadhi ya wabunge wa chama cha mapinduzi CCM kutoka Tanzania bara na visiwani wamesema watahakikisha serikali inashirikiana na Kuchauka kutatua changamoto hizo baada ya wakazi hao kumpa ridhaa ya kuongoza jimbo hilo.

Kwa upande wake mgombea huyo ZUBERI KUCHAUKA amesema akipata ridhaa ya kuwatumikia wananchi hao atahakikisha anaondoa changamoto hizo huku mjumbe wa halmashauri kuu mkoa wa lindi Abbasi Matulilo amewahakikishia usalama wananchi watao itokeza kupiga kura siku ya uchaguzi huo.

Uchaguzi huo mdogo wa nafasi ya ubunge katika jimbo la liwale mkoani lindi unatarajia kufanyika 0ctoba 13,mwaka huu baada ya mbunge wa jimbo hilo kuhama chama cha wananchi CUF na kuhami Chama cha Mapinduzi.
Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Liwale Faith Mitambo,akiwa jukwaani kumnadi mgombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Zuberi Kuchauka katika kampeni za marudio ya uchaguzi mdogo wa nafasi ya ubunge jimbo la liwale mkoani lindi iliyofanyika katika kata ya Nambinda jimboni humo.
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Lindi wakiwa na mgombea ubunge kupitia chama hicho zuberi kuchauka wakiwa katika kata ya Nambinda jimbo la Liwale katika kampeni za kumnadi mgombea huyo.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Singida kupitia Chama cha mapinduzi CCM Martha Moses akiwa katika kampeni za kumnadi mgombea ubunge jimbo la Liwale mkoani lindi kupitia chama hicho Zuberi Kuchauka katika kampeni za marudio ya uchaguzi mdogo katika kata ya Nambinda jimboni humo.

Mgombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi CCM jimbo la Liwale Zuberi Kuchauka akipeana mikono na Mbunge mstaafu wa jimbo hilo Faith Mitambo katika kampeni za marudio ya uchaguzi wa nafasi hiyo katika kata ya Nambinda jimboni humo

Baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM wakitumbuhiza na band ya TOT katika kampeni za kumnadi mgombea ubunge jimbo la Liwale mkoani Lindi kupitia chama hicho zuberi kuchauka katika kata ya Nambinda jimboni humo

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad