HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 11 October 2018

Wananachi wa Mikoa ya Nyanda za juu kusini watakiwa kushiriki maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
BARAZA la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limewataka wananchi wa Mikoa Nyanda za Juu Kusini kushiriki maonyesho ya bidhaa za wajasiriamali na huduma za mitaji yatakayo fanyika katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe mjini Mbeya kuanzia tarehe 19 hadi 23, Octoba, 2018 ili kujionea fursa za uwezeshaji kuelekea katika uchumi wa viwanda.

Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Bi. Beng’i Issa alisema hayo jana jijini Dar es Salaam kuwa maonyesho hayo hayo ni ya bidhaa za wajasiriamali na huduma za mitaji na yatafunguliwa na Waziri Kassim Majaliwa Octoba 20, 2018 na ambayo yanalenga kunadi fursa za uwezeshaji.

“Maonyesho haya yatawezesha upanuaji wa wigo wa masoko ya wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa za mikono kwa kutumia mali ghafi za Tanzania,” na hiyo inatoa hamasa kwa wananchi kujikita katika viwanda vidovidogo.

Baraza limeshirikiana na Mifuko ya Uwezeshaji, Vikundi vya kifedha na program za serikali za uwezeshaji kuandaa maonyesho hayo na yatafungwa na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Bw. Charales Mwijage, aliongeza kusema,Bi. Issa. 

Pia itachochea ukuaji wa sekta ya viwanda nchini, na aliongeza kusema maonyesho hayo ni ya pili kufanyika na kwa mwaka huu yana kauli mbiu isemayo ‘Mifuko ya Uwezeshaji, Program na Vikundi vya Kifedha ni chachu ya Maendeleo ya viwanda. 

“Tunatambua Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wazalishaji wakubwa wa mazao ya kilimo”, wananachi wa mikoa hii wafike kujionea fursa za mifuko ya uwezeshaji na program za serikali na  vikundi vya kifedha vilivyopo katika maeneo yao.

Bi.Issa alifafanua kwamba serikali ina mifuko 37 na ina program tatu za uwezeshaji na mifuko hiyo ipo inayotoa mikopo, ruzuku na inayoongeza ukwasi katika mabenki na serikali inahitaji kuona watu wake wanaanzisha viwanda vidogovidogo.

Alisema mifuko hii pia imejielekeza katika kuona mazao ya kilimo yaongezwe thamani na siyo kuuza mali ghafi kwa jili ya kupanua pato la mkulima na kuondoa wimbi la vijana kukimbilia mijijni kusaka ajira.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF), Bi. Haigath Kitala alisema maonyesho hayo pia yatatoa fursa kwa wajasiriamali walionufaika na mitaji ya mifuko hiyo kuonyesha bidhaa zao na wao kubadilishana mawazo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa. 

 “Maonyesho haya ni chachu ya juhudi zinazofanya na serikali katika kujenga uchumi wa viwanda vidovidogo,” na hii itawafanya watanzania kushiriki katika uchumi wao, aliongeza kusema,Bi Kitala. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo Tanzania (PASS),Bw. Nicomed Bohay aliitaka sekta binafsi kuitumia mifuko hiyo kupata mitaji na kuanzisha viwanda hasa vinazosindika mazao ya kilimo, mifugo,  na asali. 

“Kuwekeza katika maeneo hayo kutasaidia kuongeza mapato, mitaji ipo na inapatikana katika mifuko hii”, jambo la msingi wajenge tabia ya kuitumia mifuko hiyo ambayo imeundwa kwa ajili yao na kunahitajika kuwepo kwa kilimo chenye tija.

Mwenyekiti wa VICOBA FETA,Bw. Filbert Sambali alisema vicoba ni vikundi vya kuweka akiba na kukopa kuwekeza hivyo wananchi wafike katika maonyesho hayo kuona kazi ya vicoba lakini pia njia bora ya kusimamia vicoba vyao.

“Tunahitaji kuona vicoba vinakuwa sehemu ya kusaidia Tanzania kuingia katika uchumi wa viwanda kwa kuanza na viwanda vidogovidogo,” na hiyo inawezekana na itaondoa umasikini miongoni mwa wananchini sababu vikundi hivyo vipo kila sehemu ya nchi.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Bengi Issa wa pili kushoto akisisitiza jambo wakati walipokuwa akizungumza kuhusu maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji, Taasisi za Vikundi vya Kifedha na program za uwezeshaji yatakayo fanyika Viwanja vya Ruanda Nzovwe Mbeya kuanzia tarehe 19 hadi 23 octoba 2018, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS), Bw. Nicomed Bohay, kushoto mwakilishi wa IR-VICOBA, Bi. Augustina Mosha na wa pili kusho ni Mwenyekiti wa VICOBA FETA,Bw. Filbert Sambali. (Picha na Mpiga Picha wetu, Dar es Salaam).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad