HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 3, 2018

WAHAMIAJI HARAMU 298 WAMEKAMATWA MKOANI TANGA

WAHAMIAJI haramu 298 wamekamatwa mkoani Tanga kutoka nchi mbalimbali ambao waliingia nchini kinyume cha kisheria na hivyo kujikuta mikononi mwa vyombo vya dola.

Hayo yalisemwa na Afisa Uhamiaji Mkoani Tanga Ali Dady wakati akizungumza na mtandao huo ofisini kwake kuhusu wahamiaji haramu waliokamatwa kwa kipindi cha kuanza Januari hadi Agosti mwaka huu.

Alisema mwezi January walikamatwa wahamiaji haramu 49 ambao walikuwa wametoka kwenye nchi mbalimbali ikiwemo Somalia,Kenya,Tanzania na China huku kwa mwezi February wakimatawa 77 kutoka nchi za Somalia,Ethiopia, Burundi,Uganda,Kenya na Paskistani.

Afisa Uhamiaji huyo alisema katika mwezi Machi na Aprili idadi yao uingiaji wa wahamiaji hao ulishuka ambapo Machi walikamatwa 18 na Aprili walikamatwa 26 huku mwezi Mei wimbi la ukamataji wao liliongezeka.

“Kwa mwezi Mei walikamatwa wahamiaji haramu 94 kutoka kwenye nchi za Ethiopia, Congo, China na Somalia huku mwezi June na Julai wakikamatwa wahamiaji 12 “Alisema.

Hata hivyo alieleza kwamba katika mwezi Agosti mwaka huu walimatwa wahamiaji haramu 22 kutoka nchi za Ethiopia,Kenya,Somalia na Tanzania ambao wamekuwa mawakala wa wahamiaji hao.

Alisema idadi ya wahamiaji kuingia mkoani Tanga imekuwa ikipungua kila wakati kutokana na kuwepo kwa ufuatiliaji sambamba na kuwekwa vizuizi kwenye maeneo mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad