HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 29, 2018

TADB, YARA kuendelea kuchagiza tija katika uzalishaji wa kilimo

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imekubaliana na Kampuni YARA Tanzania kuendelea kuchagiza tija katika uzalishaji katika mazao ya kimkakati ya kilimo hapa nchini.

Dhamira hiyo ya kuwasaidia wakulima imewekwa wazi wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine na Meneja Mkuu wa YARA Tanzania, Bw. William Ngeno kilichofanyika katika Ofisi za YARA jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho, Bw. Justine amesema kuwa Benki ya Kilimo imejidhatiti kuwasaidia wakulima wadogo wadogo nchini kwa kuchagiza uzalishaji ili kuongeza kipato kwa wakulima hao.

“Tumedhamiria kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka  kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kuongeza kipato kwa wakulima wadogo nchini,” alisema.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa YARA Tanzania, Bw. William Ngeno alisema kuwa uhakika wa mbolea bora na viuatilifu vya uhakika ni muhimu katika kuongeza tija na uzalishaji hali itakayochochea kuongeza kipato cha mkulima nchini.

Aliongeza kuwa matumizi ya pembejeo bora ni msingi katika mapinduzi ya kilimo kama inavochagizwa na TADB.

“Matumizi bora ya pembejeo yanasaidia kuongeza tija katika kilimo hivyo kuleta uhakika wa mavuno kwa wakulima wadogo wadogo” alisema.
 Meneja Mkuu wa YARA Tanzania, Bw. William Ngeno (kushoto) akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) wakati walipokutana kuzungumzia mikakati ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo nchini. Wengine pichani ni maofisa kutoka TADB na YARA Tanzania.
 Meneja wa Utafiti wa Udongo wa YARA Tanzania, Bw. Peter Assey (kulia) akitoa maelekezo ya namna wanavyofanya utafiti wa udongo ili kubaini mbolea sahihi kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo hapa nchini. Wanaomsikiliza ni Meneja wa Wakulima Wadogo kutoka TADB, Bw. Joseph Mabula (kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (katikati) na Meneja Mkuu wa YARA Tanzania, Bw. William Ngeno (wapili kulia)
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine na timu yake wakiangalia namna mbolea inavyofungwa tayari kwenda sokoni.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) akizungumza wakati wa ukaguzi wa shughuli za uzalishaji wa mbolea unaofanywa na Kampuni ya YARA Tanzania. Pichani ni Meneja Mkuu wa YARA Tanzania, Bw. William Ngeno (kushoto), Meneja wa Wakulima Wadogo kutoka TADB, Bw. Joseph Mabula (wapili kushoto) na Meneja wa Utafiti wa Udongo wa YARA Tanzania, Bw. Peter Assey (kulia).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (wa pili kushoto) akisikilza maelezo kuhusu aina ya mbolea zinazozalishwa na Kampuni ya YARA Tanzania. Anayetoa maelezo hayo ni Meneja Mkuu wa YARA Tanzania, Bw. William Ngeno (kushoto). Wengine pichani ni Meneja wa Wakulima Wadogo kutoka TADB, Bw. Joseph Mabula (wapili kulia) na Meneja wa Utafiti wa Udongo wa YARA Tanzania, Bw. Peter Assey (kulia).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad