HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 16, 2018

SHIRIKA LA DAWA ASILIA NA ULINZI WA MAZINGIRA WAWAASA WATANZANIA KUWAENZI WAASISI WA TAIFA LA TANZANIA

Na Khadija Seif, Globu ya Jamii

Katika kumbukizi ya miaka 19 ya Muasisi wa Taifa la Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage nyerere   ambae alifanikisha kupatikana kwa uhuru mnamo mwaka 1960 wadau pamoja na  Shirika la dawa asilia na ulinzi wa mazingira (TRAMEPRO) wamefanya dua katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

Aidha Mkurugenzi wa shirika la dawa asilia na ulinzi wa mazingira  (TRAMEPRO) Simba simba ameeleza lengo la kudhuru makaburi hayo ni kumuenzi marehemu Kingunge Ngombale Mwiru ambae walishirikiana na hayati nyerere katika kujikomboa Kwenye utumwa na kufanikisha kupatikana kwa uhuru na kuifanya nchi ya Tanzania kuwa ya mshikamano na Umoja.

Aidha , Simba amepongeza juhudi zinazofanywa na serikali ya Mapinduzi ya awamu ya nne chini ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ameweza kuiga mifano,uchapakazi na ushupavu  ambao alikua akifanya Muasisi huyo.

Hivyo basi vijana pamoja na viongozi hawana budi kuwaenzi waasisi ambao wametoa mchango mkubwa katika kulijenga,kulitetea na kuimarisha Muungano kwa ajili ya Mustakabali wa Taifa letu kwa ujumla.

Pia. Ametoa rai kwa viongozi wengine kuwaenzi waasisi hao ambao walileta uhuru na kuifanya nchi iwe ya amani hivo basi tujitahidi kulinda amani hiyo ambayo ikipotea ni madhara kwetu sote.

Katibu Mkuu wa Shirika la dawa asilia na ulinzi wa mazingira  (TRAMEPRO) Bonaventura Mwarongo ameeleza mchango wa Kingunge Ngombale Mwiru  aliteuliwa kwenda London uingereza kuuchukua mwili wa hayati Kambarage nyerere   na Kuuleta Tanzania.

Mwarongo ameeleza licha ya kushirikiana Kwenye jitihada za kulitetea Taifa pia ngombali  alikua mlezi kwa chama cha dawa asilia na kuhakikisha wanapewa vipaumbele katika kuleta chachu Pamoja kuwawekea mikakati sahihi ya kutoa huduma zao na kueka sheria za utoaji wake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad