HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 1, 2018

SERIKALI YAWAAGIZA WENYEVITI WA VIJIJI KUSIMAMIA WAKANDARASI MIRADI YA UMEME VIJIJINI

Na Veronica Simba – Lindi
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewaagiza Wenyeviti wa Vijiji nchini kote, ambako miradi ya umeme vijijini inatekelezwa, kuwasimamia wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo ili wakamilishe kazi kwa wakati.
Alitoa maagizo hayo kwa nyakati tofauti Septemba 27 mwaka huu, akiwa katika ziara ya kazi katika vijiji mbalimbali vya Mkoa wa Lindi ambako aliwasha rasmi umeme na kuzungumza na wananchi.
Katika kuhakikisha maagizo yake yanatekelezwa, Waziri Kalemani aliwataka wakandarasi kuripoti kila siku asubuhi kwa wenyeviti wa vijiji husika, ambako wanatekeleza miradi ili kujiridhisha kuwa wapo kazini.
Aidha, Waziri aliwataka wenyeviti hao kujiridhisha kuwa wakandarasi husika hawaajiri vibarua kutoka nje ya maeneo yao bali watoke katika vijiji husika. “Mwenyekiti ukigundua kuwa Mkandarasi kaajiri vibarua kutoka nje, mtaarifu Mkuu wa Wilaya mara moja ili achukue hatua stahiki.”
Vilevile, aliwaagiza Mameneja wa TANESCO wa Kanda na Wilaya kuongeza nguvu katika zoezi hilo la kuwasimamia wakandarasi ili kuhakikisha wanafanya kazi ipasavyo.
Akiwa mkoani Lindi, Waziri kalemani aliwasha umeme katika vijiji vya Chipande (Lindi Vijijini), Luchelegwa (Luangwa) na Legezamwendo (Liwale).
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chipande, Kata ya Rondo, Lindi Vijijini, akiwa katika ziara ya kazi Septemba 27, 2018 ambapo pia aliwasha rasmi umeme katika eneo hilo.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akiwasha umeme katika Jengo la Kituo cha Afya cha Rondo, Lindi Vijijini, Septemba 27, 2018 kuashiria uwashaji rasmi wau meme katika eneo hilo. Wanaoshuhudia tukio hilo ni viongozi mbalimbali wa Serikali na wananchi wakiongozwa na Mbunge na Waziri Mstaafu Benard Membe.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (kushoto) akijadiliana jambo na Mbunge na Waziri Mstaafu Benard Membe, kabla ya kuwasha rasmi umeme katika Kijiji cha Chipande, Kata ya Rondo, Lindi Vijijini. Tukio hilo lilifanyika Septemba 27, 2018.
 Mbunge na Waziri Mstaafu Benard Membe, akizungumza wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika Kijiji cha Chipande, Kata ya Rondo, Lindi Vijijini. Tukio hilo la kuwashwa rasmi umeme katika eneo hilo lilifanywa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (mwenye shati la bluu-walioketi), Septemba 27, 2018.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani na Waziri Mstaafu Benard Membe (mbele), wakiwa wameongozana na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi, kuelekea kwenye Kituo cha Afya cha Kata ya Rondo, Lindi Vijijini ambapo Waziri aliwasha rasmi umeme katika eneo hilo. Tukio hilo lilifanyika Septemba 27, 2018.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati), akizungumza na wananchi wa Kata ya Rondo, Lindi Vijijini, wakati wa hafla ya kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo. Tukio hilo lilifanyika Septemba 27, 2018.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati), akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Luchelegwa, Wilaya ya Luangwa, Mkoa wa Lindi, wakati wa hafla ya kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo. Tukio hilo lilifanyika Septemba 27, 2018.
 Wananchi wa Kijiji cha Legezamwendo, Wilaya ya Liwale, Mkoa wa Lindi wakishangilia mara baada ya Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo. Tukio hilo lilifanyika Septemba 27, 2018.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (kulia) akimkabidhi kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Sarah Chiwamba (kushoto), wakati wa hafla ya kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo. Tukio hilo lilifanyika Septemba 27, 2018.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akikata utepe katika Jengo la Kituo cha Afya kuashiria uwashaji rasmi wa umeme katika Kijiji cha Luchelegwa, Wilaya ya Luangwa, Mkoa wa Lindi. Tukio hilo lilifanyika Septemba 27, 2018.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad