HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 18 October 2018

SERIKALI KUREJESHA HALI YA WANANCHI KUJILETEA MAENDELEO

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipokea Maelezo ya Mradi wa ujenzi ya Shule Shikizi iliyopo kata ya Mwambao Kijiji cha Mweyubaruti Kibiti Mkoani Pwani.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipokea mchango wa ujenzi wa shule ya Mradi wa ujenzi ya Shule shikizi iliyopo kata ya Mwambao Kijiji cha Mweyubaruti Kibiti Mkoani Pwani kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikabidhiwa  mabati kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa shule shikizi iliyopo katika Kijiji cha Meyebaruti  kilichopo katika Kata ya Bungu Kibiti Mkoani Pwani. Picha Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Na Mwandishi Wetu Kibiti, Pwani
Wananchi wa Kijiji cha Mweyubaruti Kata ya Mwambao Wilaya Kibiti wametakiwa kujenga hali ya kujiletea maendeleo badala ya kusubiri serikali kwakuwa mwelekeo wa serikali ni kurejesha hali iliyopotea  ya wananchi kuchangia   maendeleo yao wenyewe. 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile amesema hayo wakati alipotembelea Kijiji hicho kujionea shughuli za wananchi kujiletea  maendeleo.

"Zamani wananchi walikuwa wanajenga shule wao wenyewe au kushiriki kwa kujitolea nguvu zao na serikali inataka kurejesha hali hii na huu ndio mwelekeo wa serikali". Alisema Dkt.Ndugulile.

Wananchi kwa kutumia nguvu juhudi zao wamefanikiwa ku 
anzisha  mradi wa  shule shikizi kwa ajili ya watoto wadogo ambao hawawezi kwenda umbali mrefu kuhudhuria masomo ya awali.

Wakati huhuo Katibu wa Kitongoji Kijiji hicho Bw. Alfan Matimbo akitoa taarifa Kwa Naibu Waziri Ndugulile  kuhusi  taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo alisema wanafunzi wamekuwa wakishindwa kuhudhulia masomo katika shule ya  Msingi Kivinje B kutokana umbali mrefu kwani shule hiyo iko umbali wa km.5 kutoka Kijijini hapo.

Aidha Mzee Matimbo aliongeza kuwa umbali wa Kijiji hicho na shule ya Msingi Kivinje B ni chanzo cha utoro kwa watoto wa Kijiji chake  lakini pia wanafunzi wengi wamekatiza masomo hivyo wananchi wamejipanga kujenga shule ili kuwezesha watoto wao kuendelea na masomo.

Aidha katika juhudi za kupambana na tatizo hilo Kijiji kinamlipa mwalimu wa kujitolea ambaye analipwa sh. 1500 kwa kaya kwa mwezi lakini pia wale wanaoshindwa kutoa fedha hii uchangia mazao ya chakula kama miogo na nanasi.

Vilevile Kijiji chake kimechanga fedha na kumwezesha mwalimu huyo kwa kumnunulia baiskeli ili aweze kumudu kusafili umbali huo kwa ajili ya kufundisha watoto wao.

Mpaka sasa ghalama za ujenzi wa Jengo la shule ni kiasi cha Tsh.milioni sita lenye mahitaji ya mabati 120 na Naibu Waziri Ndugulile ametoa zawadi ya mabati 35 kuchangia juhudi zao kujiletea maendeleo.

Wakati huo huo pia Naibu Waziri Ndugulile pia amezitaka Halmashauri zote Nchini kuitikia agizo la serikali la kutenga asilimia kumi ya mapato zake kwa ajili kusaidia vikundi vya vijana, wanawake na walemavu.

Aidha Naibu Waziri alichanganua matumizi ya kiwango hicho cha mapato kuwa wanawake na vijana kwa kundi moja ni asilimia nne na asilimia mbili ni kwa ajili ya walemavu.

Naibu Waziri Ndugulile yuko mkoani Pwani katika ziara ya siku mbili kukagua na kujionea miradi ya    maendeleo inayotekelezwa na wananchi kujikwamua kiuchumi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad