HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 18, 2018

NDITIYE AKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI A BANDARI KAVU, KWALA VIGWAZA

 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa bandari kavu, Kwala eneo la Vigwaza mkoani Pwani. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Mhandisi Charles Otare na wa kwanza kulia ni Meneja wa Mradi huo kutoka SUMA JKT Raymond Kweka.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyesimama katikati) akipata maelezo kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa bandari kavu, Kwala mkoani Pwani kutoka kwa Mkurugenzi wa huduma za Uhandisi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mhandisi Charles Ogare (anayetoa maelezo). Wa kwanza kulia ni Meneja wa Mradi huo kutoka SUMA JKT, Raymond Kweka.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akipitia ramani ya mpangilio wa matumizi ya eneo la bandari kavu, Kwala mkoani Pwani wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bandari hiyo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mhandisi Charles Ogare.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa bandari kavu, Kwala kuhusu eneo la njia ya reli itakayoingia bandarini humo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bandari hiyo mkoani Pwani. Wa kwanza kulia Kaimu Meneja wa Badari ya Dar es Salaam, Fred Liundi na wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Mhandisi Charles Ogare.
Muonekano wa eneo linaloandaliwa kujenga njia ya reli kwa ajili ya kusafirisha mizigo inayoingia na kutoka bandari kavu, Kwala mkoani Pwani wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad