HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 11 October 2018

Mo Dewji atekwa leo jijini Dar, Polisi wathibitisha

*Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar waanza msako kuhakikisha anapatikana

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii.

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limethibitisha tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara tajiri na maarufu nchini Mohamed Dewji 'Mo'.

Mo ametekwa leo mapema asubuhi akiwa katika Hoteli ya Collessium jijini Dar  es Salaam ambako alikwenda hotelini hapo kwa ajili ya kufanya mazoezi.

Kwa mujibu wa Jeshi hilo kwa sasa wanaendelea kushughulikia suala hilo kuhakikisha Mo anapatikana na linaamini lazima apatikane.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema jeshi lake tayari limeanza kufuatilia kutekwa kwa Mo Dewji .

Wakati huo huo Kamanda wa Polisi Kanda Mkoa wa Kinondoni Jumanne Muliro amesema jeshi hilo linaweledi wa kutosha katika kufanya kazi na hivyo wanaamini waliohusika kufanya utekaji huo watafahamika.

"Jeshi letu naliaminia sana kwa weledi hata saa 6 mchana haifiki Mo atakuwa amepatikana, sina wasiwasi kabisa katika hilo," amesema.

Tukio hilo la kutekwa kwa Mo limezua maswali mengi na hofu miongoni mwa Watanzania .

Mo Dewji ambaye ni mfadhili mkubwa wa Klabu ya Simba na mmoja ya wafanyabiashara matajiri barani Afrika anajulikana na makundi ya watu mbalimbali na hasa mashabiki wa soka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad