HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 31, 2018

Milioni 151 zatumika kuongeza nguvu ya kupambana na Ukimwi Rukwa

Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa kwa kushirikiana na mradi wa Military HIV Research Program (MHRP) imenunua gari aina ya Land Cruiser Hardtop kwaajili ya shughuli zinazohusiana na mapambano dhidi ya Ukimwi.

Gari hiyo ambayo alikabidhiwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Bw.Msongela Palela na mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo imenunuliwa kutokana na fedha zilizovuka mwaka 2016/2017 ikiwa ni makubaliano baina ya katibu tawala na mradi juu ya fedha zilizovuka mwaka kupangiwa matumizi yanayolenga kuboresha huduma za Ukimwi.

Wakati akikabidhi gari hiyo Mh. Wangabo alitahadharisha matumizi ya gari hiyo huku akipiga mfano wa gari ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) ya halmashauri ya Wilaya ya Kalmabo iliyokuwa na mazoea ya kwenda kwenye sehemu za starehe kuwa mshauri wa mradi huo tayari ameshachukuliwa hatua za kinidhamu.

“Tarehe 7 mwezi wa 10 gari hii tulilishika hapa Sumbawanga likiwa eneo la starehe na huyo mshauri wa mradi huo ndiye aliyekuwa anaendesha gari hilo, tulichukua hatua kali za kumuondoa na kumrudisha kwa mwajiri wake kwaajili ya hatua nyingine za kinidhamu, nitoe wito kwa madereva wa serikali kutumia magari kwa mambo yao binafsi, suala hili lisijitokeze, hatua kali zitachukuliwa,” alisisitiza.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi wa mradi huo Bw. Riziki Kasimu ameshukuru ushirikiano anaoupata kutoka katika halmashauri na serikali ya Mkoa ili kuhakikisha wanashusha na kutokomeza maambukizi ya Ukimwi na ameiomba serikali ya Mkoa wa Rukwa kutoa kipaumbele kwa kazi za Ukimwi katika matumizi ya gari.

“Pamoja na Kazi zote zilizopo Mkoani, tungependa kazi za mradi zipewe kipaumbele katika matumizi ya gari, ni kweli kwamba tuna kazi nyingi ama majukumu mengi ambayo hayo magari yangepaswa kufanya na sisi kama washirika kwenye maendeleo hatuwezi kusema gari hili litumike moja kwa moja kwa Ukimwi tu, lakini pale tunapokuwa na majukumu ya msingi ya Ukimwi tungependa msisitizo utolewe huko,”Alisema.

Mtadi huo tayari umeshatoa gari 7 katika Mkoa wa Rukwa, 4 katika Halmashauri zote za Mkoa na 3 katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa jambo lililosaidia kurahisisha shughuli za kupambana na maambukizi ya Ukimbwi na hatimae kushuka kutoka asilimia 6.2 mwaka 2015 hadi asilimia 4.4 mwaka 2018. 
 Mwakilishi wa Mradi wa MHRP Bw. Riziki Kasimu (kulia) akimkabidhi funguo za gari litakalotumika kuongeza nguvu za mapambano dhidi ya maambukizi ya Ukimwi kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) mbele ya wadau dhidi ya maambuzi hayo. 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo akiwasha gari lililokabidhiwa kupitia ushirikiano wa Ofisi yake na Mradi wa MHRP kwaajili ya mapambano dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.
 Gari aina ya Land Cruiser Hardtop lililokabidhiwa kwa halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kwaajili ya kuongeza nguvu ya mapambano dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad