HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 15, 2018

Mesen Selekta na Gutta wapagawisha Tigo Fiesta -Vibe Kama Lote Mtwara

Msanii Jerry Boniface maarufu kama Mesen  Selekta akishirikiana na mdogo wake Gutta waliweza kuwapagawisha mashabiki kwa mtindo wao Singeli. Msanii huyo alidhihirisha ubora wake uliopelekea uwanja kutimka vumbi kwa nyimbo zake za Kinanda, Kanyaboya, Dab Singeli na nk.
Mji wa Mtwara ulikuwa tofauti na miji mingine kutokana na wasanii kuimba pamoja na mashabiki.

Akizungumza na waandishi wa habari Mesen Selekta alisema " Hii inanipa mzuka kwa mashabiki kuukubali muziki wangu, nimeona jinsi shangwe la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote walivyolipokea wana Mtwara".
Msanii mwingine aliyeiteka Mtwara alikuwa Farid Kubanda Fid Q aliwaamsha kwa wimbo wake Fresh, ambao aliurudia mara mbili kutokana na kiu ya mashabiki.
Kivutio kingine kilikuwa kwa MaDj  Zero na Mafuvu waliweza kupiga mziki kwa zamu kama kwa kushindana hii iliweza kuleta ladha na Vibe la aina yake kwa mashabiki.
Kila Tamasha linapopita utafutwa msanii Chipukizi kupitia shindano la kusaka vipaji vya wasanii maarufu Kama Tigo Fiesta Supa Nyota, na kwa mkoa huo msanii, Siraji Mbuta kwa jina la kisanii Mbuta The Swagx aliibuka kidedea kuwakilisha mkoa huo kwenye fainali mwezi ujao.

Kwa upande wa wadhamini Kampuni ya Tigo, Meneja wa Kanda ya Pwani, John Tungaraza alisema ‘Mbali na muziki, wateja wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi mara mbili ya thamani kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia *147*00#. Promosheni ya Data Kama Lote itahakikisha kuwa mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio yote ya msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi kwenye mtandao wenye kasi zaidi wa 4G+,’ Tungaraza alisema.
Wateja wote wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi TSH 10 millioni, zawadi za kila wiki za TSH milioni moja, ama zawadi za kil asiku za TSH 100,000 kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo. Ushiriki katika shindano hilo unapatikana kwa kutuma neno MUZIKIkwenda 15571 au kwa kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz.

Walioshusha vibe kama lote mjini Mtwara ni pamoja na kundi la Rostam (Roma and Stamina), Fid Q, Zaid na Weusii (Joh Makini, Niki wa Pili na G-Nako) ambao walikonga mioyo ya wapenzi wa muziki mjini Songea pia. Wengine ni wasanii wa bongo flava Mesen Selekta na Foby, wakongwe Chegge, Barnaba na Mr Blue, pamoja na akina dada Ruby na Lulu Diva.

TIketi za Tigo Fiesta 2018 – zitakuwa zinapatikana  kupitia Tigo Pesa Masterpass QR kwa kupiga *150*01#, kuchagua namba 5 (lipia bidhaa), na kuchagua namba 2 (lipa kwa Masterpass). Tuma kiasi husika  kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Msanii Chege kutoka TMK Family akionesha uwezo wake wa kutawala jukwaa kwenye Tamasha kubwa la Tigo Fiesta -Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Nang'wanda Mjini Mtwara usiku wa kuamkia Jumatatu.
Msanii Lulu Diva akionesha uwezo wake wa kutawala jukwaa kwenye Tamasha kubwa la Tigo Fiesta -Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Nang'wanda Mjini Mtwara usiku wa kuamkia Jumatatu.
Mshindi atakayeiwakilisha Mtwara kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka Tigo Fiesta Supa Nyota, Siraji Mbuta a.k.a Mbuta The Swagx akionesha uwezo wake kwenye jukwaa la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jumatatu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad