HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 30 October 2018

Makamu wa Rais atembelea Banda la IPP TOUCHMATE wiki ya maonyesho ya Viwanda Kibaha Inbox x

Makamu wa Rais atembelea Banda la IPP TOUCHMATE wiki ya maonyesho ya Viwanda Kibaha
Na Mwandishi wetu,
Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan jana amezindua wiki ya maonyesho ya viwanda ambapo taasisi 25 zinashiriki kuonyesha  bidhaa zake huku yakibeba kauli mbiu ya ‘Viwanda Vyetu, Uchumi Wetu’ yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani.
Kabla ya kutoa hotuba yake katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais alitembelea banda la kampuni ya IPP TOUCHMATE na kupata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makapuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi.
Dk. Mengi alimweleza Makamu wa Rais kuhusu ushirikiano wa kampuni hizo mbili wa kuanzisha kiwanda cha kutengeneza vifaa mbalimbali vya Kielekroniki nchini vitakavyouzwa kwa bei nafuu na kutumika katika utoaji wa elimu, ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu wa tano ya kuboresha  elimu.
Dk. Mengi alimweleza Makamu wa Rais kuwa kampuni ya Touchmate ipo Dubai na ina uzoefu wa miaka 30 wa kutengeneza vifaa vya kielektroniki kama simu za kisasa (smart phones, tablets, kompyuta na vifaa vya nyumbani).
 Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi akisalimiana na mgeni rasmi Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan alipowasili katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani kwa ajili ya kufungua wiki ya maonyesho ya viwanda ambapo taasisi 25 zinashiriki kuonyesha  bidhaa zake huku yakibeba kauli mbiu ya ‘Viwanda Vyetu, Uchumi Wetu’. 
 Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi akiteta jambo na mgeni rasmi Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan alipowasili katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani kwa ajili ya kufungua wiki ya maonyesho ya viwanda ambapo taasisi 25 zinashiriki kuonyesha  bidhaa zake huku yakibeba kauli mbiu ya ‘Viwanda Vyetu, Uchumi Wetu’. 
 Mgeni rasmi Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwasisi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Touchmate, Bw. Vasant Menghani alipowasili katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani kwa ajili ya kufungua wiki ya maonyesho ya viwanda ambapo taasisi 25 zinashiriki kuonyesha  bidhaa zake huku yakibeba kauli mbiu ya ‘Viwanda Vyetu, Uchumi Wetu’.  
 Mgeni rasmi Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (kulia), alipotembelea banda la IPP TOUCHMATE katika maonyesho ya wiki ya maonyesho ya viwanda ambapo taasisi 25 zinashiriki kuonyesha  bidhaa zake huku yakibeba kauli mbiu ya ‘Viwanda Vyetu, Uchumi Wetu’. Kushoto ni Mwasisi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Touchmate, Bw. Vasant Menghani.
 Mgeni rasmi Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan akikagua vifaa vya kielektroniki kama simu za kisasa (smart phones, tablets, kompyuta na vifaa vya nyumbani) huku akipata maelezo kutoka kwa mwasisi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Touchmate, Bw. Vasant Menghani (kushoto) alipotembelea banda la IPP TOUCHMATE katika maonyesho ya wiki ya maonyesho ya viwanda ambapo taasisi 25 zinashiriki kuonyesha  bidhaa zake huku yakibeba kauli mbiu ya ‘Viwanda Vyetu, Uchumi Wetu’. Kushoto ni Mwasisi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Touchmate, Bw. Vasant Menghani. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa  IPP Touchmate, Bw. Victor Tesha na wa pili kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi.
 Mgeni rasmi Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan akisoma maelezo yaliyomo kwenye moja ya bidhaa za kielektoniki alipotembelea banda la IPP TOUCHMATE katika maonyesho ya wiki ya maonyesho ya viwanda ambapo taasisi 25 zinashiriki kuonyesha  bidhaa zake huku yakibeba kauli mbiu ya ‘Viwanda Vyetu, Uchumi Wetu’. Kushoto ni mwasisi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Touchmate, Bw. Vasant Menghani.
Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la IPP Ltd lililopo katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani  wakiangalia vifaa vya kielektroniki kama simu za kisasa (smart phones, tablets, kompyuta na vifaa vya nyumbani) wakati wa ufunguzi wa wiki ya maonyesho ya viwanda ambapo taasisi 25 zinashiriki kuonyesha  bidhaa zake huku yakibeba kauli mbiu ya ‘Viwanda Vyetu, Uchumi Wetu’, yaliyofunguliwa rasmi jana na Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan mkoani humo.
 Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (kushoto) akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Nishati, Mh. Subira Mgalu wakati wakisubiri kuwasili kwa mgeni rasmi Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani kwa ajili ya kufungua wiki ya maonyesho ya viwanda ambapo taasisi 25 zinashiriki kuonyesha  bidhaa zake huku yakibeba kauli mbiu ya ‘Viwanda Vyetu, Uchumi Wetu’. Katikati ni Mwasisi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Touchmate, Bw. Vasant Menghani
 Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (kushoto) na Mwasisi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Touchmate, Bw. Vasant Menghani wakiwa kwenye picha ya pamoja ndani ya banda la IPP Ltd lililopo katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani wakati wa ufunguzi wa wiki ya maonyesho ya viwanda ambayo taasisi 25 zinashiriki kuonyesha  bidhaa zake huku yakibeba kauli mbiu ya ‘Viwanda Vyetu, Uchumi Wetu’, yaliyofunguliwa rasmi jana na Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan mkoani humo.
 Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (wa pili kulia), Mwasisi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Touchmate, Bw. Vasant Menghani (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa  IPP Touchmate, Bw. Victor Tesha (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja nje ya ya banda la IPP Ltd lililopo katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani wakati wa ufunguzi wa wiki ya maonyesho ya viwanda ambayo taasisi 25 zinashiriki kuonyesha  bidhaa zake huku yakibeba kauli mbiu ya ‘Viwanda Vyetu, Uchumi Wetu’, yaliyofunguliwa rasmi jana na Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan mkoani humo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad