HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 19 October 2018

MAHAKAMA IMEWAASA MAJAJI NCHINI KUZINGATIA SHERIA ZILIZOPO KULINGANA NA MAZINGIRA

Na Karama Kenyunko, Glogu ya Jamii
MAHAKAMA imewaasa Majaji nchini kuzingatia sheria  zilizopo kulingana na mazingira ya Taifa na Jamii kwa ujumla katika mchakato mzima wa kutoa maamuzi ili kimuweza kutenda haki na usawa.

Wito huo umetolewa na majaji wastaafu wa Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, jaji Rugazia, John Mjemmas na Agathon Nchimbi wakati wa hafla fupi ya kuwaaga kitaaluma iliyofanyika mapema leo Oktoba 19.2018  katika ukumbi wa wazi wa Mahakama Kuu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Jaji Nchimbi amewakumbusha majaji na mahakimu kuhakikisha kuwa  wanakuwa waaminifu wakati wanatimiza majukumu yao kama maofisa wa mahakama ili mwisho wa Siku kila mmoja aweze kuona haki imetendeka.

Amesema, kwa kuwa mahakama ni chombo cha kutoa haki basi ni muhimu kuzingatia sheria zilizopo kulingana na mazingira ya taifa na Jamii katika mchakato mzima wa kutoa haki, Maamuzi yawe ya haki na usawa siyo tu hivyo  bali yaonekane kuwa ya haki na usawa" Amesema Jaji Nchimbi.

Aidha amewaasa  majaji wa mahakama kuzingatia matakwa ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwataka wajielekeze katika kutenda haki, kwa mujibu wa viapo walivyoapa bila ya kuwa na uoga, upendeleo wala chuki.

Naye Jaji Mjemmas amesema wakati akitimiza majukumu yake alipata ushirikiano toka kwa watu mbalimbali wakiwamo majaji, mawakili wa serikali na wa kujitegemea, mahakimu, makarani na watumishi wengine.

Amesema ingekuwa hao pengine mafanikio yake yasingeonekana na kwamba ni kitu cha kawaida katika maisha mtu akiwa anatimiza majukumu yake hawezi kumridhisha kila mtu, hivyo aliomba msamaha kwa wote.

Pia, amewaasa  majaji waliobaki kazini kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha mahakama inabaki  kuwa muhimili usio na upendeleo wa kuogopesha kitend kitakacho iweezesha Jamii kuendelea kuwa na imani nayo na hivyo kuleta ustawi katika Jamii.

Akizungunza kwa niaba ya mahakama, Jaji Clesensia Makuru amesema ukiangalia historia na namna ya waliostaafu walivyokuwa inaonesha walifanya kazi kwa uaminifu kwani kama inavyoeleweka kupata nafasi ya kuwa Jaji unatakiwa uwe na uelewa wa kutosha juu ya masuala ya sheria.

"Majaji waliostaafu watakumbukwa  kwa maamuzi mbali mbali waliyoyatoa ambayo yameleta mchango mkubwa katika maendeleo sheria hapa nchini kwani walitumia nafasi zao vizuri na muda katika kujifunza ili watimize majukumu yao ipasavyo. Amesema.

Kwa upande wake, Jaji  Kiongozi Eliezer Feleshi amesema tukio la kuagwa kwa majaji wastaafu hao kitaaluma ni kuendelea kujenga umoja wa majaji na mahakimu na kutambua kazi zao hata wanapostaafu na kuiwezesha Jamii kuzijua huku  wasifu wao ukiwapa morali waliopo kazini kufanya kazi kwa ufanisi ili kufuata nyayo zao.

Jaji Kiongozi Eliezer Feleshi, wa katikati,  wa pili kushoto ni Jaji mstaafu Agathon Nchimbi, wa pili kulia ni Jaji Gad Mjemmas, wa kwanza kulia ni Jaji wa mahakama kuu divesheni ya Arshi, jaji, Crensensia Makuru na kwa kwanza kushoto ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu divisheni ya ardhi, Rehema Kerefu wakiwa katika Picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa hafla hiyo
 Jaji kiongozi, Eliezer Feleshi wa katikati waliokaa akiwa katika Picha ya pamoja na majaji wastaafu wa Mahakama Kuu kitengo cha ardhi, na Watumishi wengine wa Mahakama Kuu mara baada ya hafla ya kuwaaga kitaaluma iliyofanyika leo katika ukumbi wa wazi  wa Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
 Jaji Kiongozi Eliezer Feleshi, wa katikati waliokaa, akiwa katika Picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa Habari walioshiriki katika hafla ya kuwaaga kitaaluma majaji waliostaafu,  wa pili kushoto ni Jaji mstaafu Agathon Nchimbi, wa pili kulia ni Jaji Gad Mjemmas, wa kwanza kulia ni Jaji wa mahakama kuu divesheni ya Arshi, jaji, Crensensia Makuru na kwa kwanza kushoto ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu divisheni ya ardhi, Rehema Kerefu. 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad