HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 4 October 2018

KAMATI YA UONGOZI YA CHAMA CHA MASPIKA WA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA KANDA YA AFRIKA(CPA-AFRIKA) MJINI ZANZIBAR

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza na Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (Mb), (Wa kwanza kushoto) na Ujumbe wake ambao ni Kamati ya Uongozi ya Chama cha Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika(CPA-Afrika) waliokwenda kumtembelea leo Ikulu Zanzibar. Wa pili kushoto ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Zuberi Ali Maulid, Naibu Spika wa Bunge la Rwanda Mheshimiwa Edda Mukabagwiza na Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai.
  Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (Mb) (kushoto) na Naibu Spika wa Bunge la Rwanda Mheshimiwa Edda Mukabagwiza (kulia) mara baada ya kuzungumza nao Ikulu Zanzibar.
 Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (Mb) akiongoza kikao cha Kamati ya Uongozi ya Chama cha Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika(CPA-Afrika)  kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Tunguu, Zanzibar. Wa kwanza kutoka kulia ni Spika wa Bunge la Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Zuberi Maulid, Spika wa Bunge la Sierra Leone Dkt. Abbas Bundu na  Naibu Spika wa Bunge la Rwanda Mheshimiwa Edda Mukabagwiza.
 Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (Mb) (wa tatu kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Wajumbe  Kamati ya Uongozi ya Chama cha Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika(CPA-Afrika. Kutoka (kushoto) kwa waliokaa ni Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai, Naibu Spika wa Bunge la Rwanda Mheshimiwa Edda Mukabagwiza, Spika wa Bunge Bunge la Sierra Leone Dkt. Abbas Bundu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Zuberi Maulid na Katibu Msaidizi wa CPA-Afrika Ndg. Demetrius Mgalami. Waliosimama ni Sekretarieti ya Wajumbe  wa  Kamati ya Uongozi ya Chama cha Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika(CPA-Afrika).
 Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Zuberi Maulid (katikati) wakati alipotembelea Baraza hilo kabala ya kuanza kwa kikao cha Kamati ya Uongozi ya Chama cha Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika(CPA-Afrika) kinachoendelea Mjini Zanzibar. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge la Rwanda Mheshimiwa Edda Mukabagwiza.

PICHA NA BUNGE

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad