HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 17, 2018

KAIMU MKURUGENZI TPA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO KUJIBU MASHTAKA MATATU

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
KAIMU Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa mamlaka ya bandari Tanzania, (TPA) Peter Gawile amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kuisababishia TPA hasara ya zaidi ya sh milioni 150.

Akisomewa hati ya mashtaka na wakili wa serikali kutoka Takukuru, Lizy Kiwia mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi imedaiwa, Oktoba 25, 2012  huko katika ofisi kuu za TPA zilizopo, Temeke mshtakiwa huyo  wakati akijua na kwa nia ya kumdanganya muajiri wake alitumia nyaraka ya malipo ya kodi (Invoice) namba MKOO/722A kutoka Kampuni ya Bob investment Ltd. 

Akidai kuwa, garama ya  semina ya siku tatu ilikuwa ni sh. 47,935,140 wakati akijua alikuwa na lengo La kumdanganya muajiri wake huyo TPA.

Katika shtaka la pili imedaiwa siku na mahali hapo mshtakiwa huyo wakati akijua na kwa nia ya kumdanganya muajiri wake alitumia nyaraka ya malipo ya kodi (Invoice) namba MKOO/722B kutoka Kampuni ya Bob investment Ltd. Akidai kuwa, garama ya  semina ya siku tatu ilikuwa ni sh. 47,935,140 wakati akijua alikuwa na lengo La kumdanganya muajiri wake huyo TPA.

Katika shtaka la tatu mshtakiwa anadaiwa, Desemba 5 2012 akiwa TPA alitumia hati ya malipo namba MKOO/1203 Kutoka huko huko Bob yenye garama ya sh, 97,178,664

Katika shtaka la nne imedaiwa kati ya Oktoba 30 na Desemba 12/2012  huko TPA, mshtakiwa kwa nia ovu aliisababishia TPA hasara ya sh 158,947,584.

Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande kwa Kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo yalimtaka kuwa na wadhamini mawili wenye barua za utambulisho.

Pia, Hakimu alisema mshtakiwa atatakiwa kuweka nusu ya fedha hizo au kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo. Kesi imeahirishwa hadi hadi Oktoba 29, 2018 kwa kutajwa na kuangalia upelelezi umekamilika au la.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa mamlaka ya bandari Tanzania, (TPA) Peter Gawile akiingia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo kujibu mashtaka matatu likiwemo la kuisababishia TPA hasara ya zaidi ya sh milioni 150.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa mamlaka ya bandari Tanzania, (TPA) Peter Gawile akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kujibu mashtaka matatu likiwemo la kuisababishia TPA hasara ya zaidi ya sh milioni 150.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad