HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 30 October 2018

IGP SIRRO AKUTANA NA IGP WA RWANDA

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Rwanda DCG Dan Munyuza, leo 30/10/2018 walipokutana katika eneo la Kirehe karibu na mpaka unaotenganisha nchi hizo mbili Tanzania na Rwanda ambapo baadae watafanya kikao cha Ujirani mwema kitakachojadili masuala mbalimbali ya kiusalama baina ya nchi hizo mbili. Picha na Jeshi la Polisi Tanzania.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (kushoto) akiwa amefuatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Rwanda DCG Dan Munyuza, leo 30/10/2018 wakivuka mpaka unaotenganisha nchi hizo mbili Tanzania na Rwanda na kuingia eneo la Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera kwa ajili ya kikao cha ujirani mwema kitakachojadili masuala mbalimbali ya kiusalama baina ya nchi hizo mbili. Picha na Jeshi la Polisi Tanzania.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Rwanda DCG Dan Munyuza, wakati wa kikao cha ujirani mwema kinachofanyika Rusumo wilayani Ngara mpakani mwa Tanzania na Rwanda leo 30/10/2018. Picha na Jeshi la Polisi Tanzania.
Kikao kikiendelea

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad