HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 8 October 2018

CASTLE LAGER KUMLETA SAMUEL ETO'O NCHINI

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
KAMPUNI ya bia ya Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Castle lager imemualika mmoja ya wachezaji bora barani Afrika Samuel Eto'o kuzindua mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira aina ya 5-A-side utakaojengwa Oysterbay jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa bia hiyo Pamela Kikuli amesema kuwa nyota huyo atashiriki katika uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa uwanja maalumu wa soka linaloshirikisha wachezaji kumi (watano kila upande) maarufu kama ‘5-A-Side soccer’ katika eneo la Oysterbay  mkabala na jengo la Coco Plaza, jirani na ufukwe wa Coco.
 
Aidha ameeleza kuwa lengo la kumleta nguli huyo wa soka barani Afrika ni kuongeza hamasa ya soka kwa wanamichezo wenye vipaji kujitokeza kushiriki katika kabumbu.

Pia amesema kuwa kama kampuni wataendelea kushiriki katika shughuli za kijamii katika kuleta maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake msemaji ya klabu ya Simba  amesema kuwa urafiki unasimama hasa katika wakati wa kuliwakilisha taifa na amewataka mashabiki wa klabu za Simba na Yanga kujitokeza kwa wingi.

Dismas Ten msemaji wa klabu ya Yanga amesema kuwa ujio wa Eto'o nchini ni heshima kubwa kwa nchi na soka kwa ujumla hivyo wananchi hasa wapenda soka ni bora wakajitokeza ili kuweza kumfahamu nguli huyo wa mpira wa miguu.

Samuel Eto'o  anayesakata kabumbu huko Qatar anatarajia kuwasili katika uwanja wa Mwalimu Nyerere Oktoba 10 na siku ya Alhamisi atatembelea mradi huo wa ujenzi wa uwanja hicho na kushiriki mazoezi na vijana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad