HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 26 October 2018

BODI YA FILAMU YAMFUNGIA WEMA SEPETU KUTOJIHUSISHA NA FILAMU KWA MUDA USIOJULIKANA

*Wema amefungiwa kufuatia kuachia video chafu zinazosambaa mitandaoni kwa sasa

Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
Bodi ya filamu ya nchini imemfungia muiguzaji wa kike Wema Abraham Sepetu anaejulikana kama Tzsweetheart kutokana na kusambaa kwa video pamoja na picha chafu Kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Joyce Fisso ameeleza kuwa wasanii ni kioo cha jamii ambao wapo kwa ajili ya kuihabarisha ,kuiasa,kuionya jamii yale yanaoendelea katika jamii.

Fisso amesema kutokana na msanii huyo Wema Sepetu kutumia Sanaa yake kukiuka maadili ,desturi na tamaduni za  kitanzania  imeamuru kumsimamisha kutojihusisha na Sanaa yoyote Ile kwa muda usiojulikana kutokana na video pamoja na picha chafu zilizosambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

Aidha Wema Sepetu amepewa adhabu hiyo kutokana na kupotosha jamii kwa ujumla na bodi umejidhihirisha kumfungia na itaendelea kumfatilia mienendo yake kwa sasa mpaka atakapojirekebisha.

Mtendaji huyo amefafanua kuwa kama bodi wamepokea msamaha ambao aliomba kwa wadau, mashabiki na tasnia nzima ya filamu ikijumuisha na bodi ya filamu kupitia waandishi na kuita baadhi ya vyombo vya habari na kukiri kosa lake inaonyesha ni wazi atajirekebisha na makosa yake kutokana na kulidhalilisha taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad