HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 3, 2018

BODI YA BARAZA LA KILIMO TANZANIA LAHITIMISHA ZIARA YAKE YA KUKAGUA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA UBIA WA KILIMO TANZANIA.






Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafasi (TPSF) Bw. Salum Shamte ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) akimuonyesha Mwenyekiti wa Baraza la kilimo Tanzania (ACT) Dkt Sinare Yusuph (katikati) Barua kutoka Benki ya Kilimo inayokataa kuwapatia Mkopo wakulima wa Kijiji cha Minepa Wilayani Ifakara kwa kile walichodai mpaka wakulima hao wawe na hati miliki ya Mashamba hayo kitu kinachotajwa kuwa si sahihi, ambapo wajumbe wa bodi wameazimia kulifanyika kazi suala hilo.
Afisa Mauzo wa Kampuni ya Lonagro inayojihusisha na uuzaji wa zana za Kilimo hifadhi Bw Ray Travas akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Baraza la Kilimo Tanzania waliofika ofisini kwake Mjini Arusha ambapo alisema bado kuna mwitikio mdogo kwa wakulima kutumia zana za kisasa katika kilimo kutokana na uzalishaji wao kuwa mdogo huku pia wakikwamishwa na bei za mazao ambazo zimekuwa chini zaidi.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafasi (TPSF) Bw. Salum Shamte ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Baraza la Kilimo Tanzania (ACT),akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania Bi Janeth Bitegeko na wakulima mbalimbali katika moja ya ziara ya wajumbe wa bodi ya ACT kukagua miradi inayosimamiwa na Ubia wa Kilimo Tanzania (TAP).
Mkurugenzi wa kampuni ya Siza Agro Processing iliyoko Mjini Mufindi inayojishughulisha na kukoboa na kupaki kwa viwango tofauti bidhaa za mchele na unga akiwaonyesha wajumbe wa Bodi bidhaa ya Mchele inayozalishwa na Kiwanda chake, ingawa kwa sasa anasema shughuli za uzalishaji katika kiwanda hicho chenye mashine za kisasa unasuasua.
Wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya baraza la kilimo wakiwa ndani ya ghala la kuhifadhia mazao lililojengwa na ACT/TAP aktika kijiji cha katurikila wialyani Mufindi Mkoani Iringa.

Kaimu Mkurugenzi wa halimashuari ya Arumeru Bi grace Mbilinyi akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Baraza la Kilimo Tanzania walipotembelea ofisini kwake ambapo ameshukuru kwa miradi inayotekelezwa na ACT wilayani humo ikiwemo ya ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao.

Mjumbe wa bodi ya bazaar la kilimo Tanzania Bw. Enock Ndondole akiwasisistiza wakulima wa kijiji cha Minepa Wilayani Ifakara Mkoani Morogoro umuhimu wa kusambaza teknlojia wanayoitumia kwenye Kilimo cha Mpunga ya Kilimo shadidi ili wakulima wengi zaidi waweze kutumia teknlojia hiyo ambayo inamfanya mkulima kupata mazao mengi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad