HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 23 October 2018

ADA ZA SHULE NA BODABODA KUTOLEWA KWA MARA YA KWANZA KUPITIA MWALIMU COMMERCIAL BANK

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MWALIMU Commercial Bank imefanya droo yake ya kwanza ya kampeni ya "Weka Akiba na Ushinde"  iliyoanza rasmi Septemba 10 mwaka huu na itaendelea mpaka Novemba 30 mwaka huu, na hiyo ikiwa na moja ya mikakati ilinayofanywa na benki hiyo hasa katika kutoa hamasa kwa wateja wao katika kujiwekea akiba.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi Mkuu wa  Mwalimu Commercial Bank (MCB,) Ronald Manongi  amesema kuwa mteja akijiwekea akiba katika akaunti yake kuanzia shilingi 30,000 na kuendelea wakati wote wa kampeni hiyo  basi atapata tiketi moja ya kuingia katika droo inafanyika kila mwezi.

"Mteja anapoweka akiba zaidi hupata nafasi zaidi na kupata tiketi nyingi zaidi na kujiweka katika nafasi ya ushindi zaidi katika droo kubwa na zawadi zitakazotolewa ni pamoja na  ada za shule na bodaboda." ameeleza Manongi.

Aidha Manongi amesema kuwa Mwalimu Commercial Bank imeanzisha akaunti ya tukutane Januari ambayo inamuwezesha mteja kujiwekea akiba kidogo kidogo ili aweze kumudu majukumu ya mwezi Januari, aidha benki hiyo ina akaunti ya nastaafu vipi ambayo huwaanda vijana kwa kuweka akiba  itakayowasaidia baada ya kustaafu na kwa wateja wanaotumia akaunti hizo wataingia kwenye droo na kujiweka katika nafasi ya kushinda ada yenye thamani ya shilingi 500,000 na bodaboda.

Pia amewaasa wananchi kuwa na utamaduni wa  kujiwekea akiba mara kwa mara kwa ajili ya matumizi ya baadae na wao wapo kwa ajili ya kuwasaidia hivyo wasisite kutembelea ofisi zao ili waweze kujipatia huduma hizo.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha biashara na masoko Valence Luteganya amesema kuwa uzinduzi wa kampeni hiyo unalenga katika kutoa bidhaa na huduma zinazolenga maslahi ya watanzania wote.

"Mwaka huu utakuwa mwaka wa neema kwa wateja wetu na tunakaribisha watanzania wote kuja kufungua akaunti ili waweze kujiwekea akiba zao na kujiweka katika nafasi za kujishindia zawadi kemkem" amesema  Luteganya.

Hii ni droo ya kwanza kufanywa na Mwalimu Commercial Bank (MCB) na imelenga kuwanufaisha wateja kwa zawadi zikiwemo bodaboda na ada za shule kupitia kampeni hiyo ya Weka akiba na ushinde na katika droo iliyofanyika leo Tatu Lyimo amejishindia ada ya shule ya shilingi 500,000 na Godian Madinda amejishindia ada ya shule kiasi cha shilingi 500,000 na bodaboda.
Mkurugenzi Mkuu wa Mwalimu Commercial Benki (MCB),Ronald Manongi akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuchezesha droo ya kwanza ya kampeni ya kuweka akiba na kushinda bodaboda na ada za shule, jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkuu wa kitengo cha biashara na masoko,Valence Luteganya.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad